Mwanasiasa
mkongwe na mmoja wa waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Hassan Nassor
Moyo (pichani) amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake mkoani Tanga.
Mzee
Moyo ambaye aliwahi kuwa Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar,
amefikwa na mauti hayo baada ya kusumbulia na maradhi kwa muda mrefu.
Taratibu za msiba huo zinaendelea huko Tanga huku mmoja wa wanafamilia akihithibitishia Diramakini juu ya kifo hicho.
Uongozi wa Diramakini Business Limited ambao ni wamiliki wa tovuti hii ya www.diramakini.co.tz unawapa ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo Watanzania wote kwa kuondokewa na kiongozi wao mstaafu. Mwenyenzi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu. Amin
Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com