Mwenyekiti wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Mwanza asema Oktoba 28 CCM itang'ara

 MWENYEKITI wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Mwanza, Comrade Davis Peter amefanya mkutano na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Chuo Cha Ufundi cha F.D.C Wilaya ya Sengerema na kuwahimiza kuchagua viongozi wote wanaotokana na chama hicho.

"Pia tuhakikishe tunatafuta kura mpya za kutosha kutoka kwa wazazi wetu na vijana wenzetu waliojiandikisha na wenye sifa za kupiga kura katika uchaguzi huu ulio mbele yetu;

Peter ametoa wito huo ikiwa kwa sasa Watanzania wanajiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Seneti, Davis Peter aliwaomba kushirikiana sana katika kazi hiyo ya kutafuta kura mpya, "kwa kuwakumbusha vijana wenzetu mazuri yaliofanywa na Serikali yetu katika chuo hiki cha F.D.C kwani Serikali ya CCM kupitia Wiraza ya Elimu chini ya Mheshimiwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli alileta chuoni hapo mamilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi wa kike na wa kiume yenye kulaza wanafunzi 160,ukarabati jengo la utawala,ujenzi wa bwalo la kisasa, ujenzi wa karakana ya kisasa na ukarabati wa jiko la kupikia chakula.

"Ila sio hivyo tu tuhakikishe tunawakumbusha Serikali inayoongozwa na CCM chini ya Rais wetu Dkt. John Pombe  Joseph Magufuli na Makamu wake Mama Samia Suluhu Hassan ndio iliyopunguza mzigo wa ada kwa wazazi wetu kutoka 780,000 hadi 250,000 kwa wanafunzi wa ndani na 245, 000 kwa wanaoishi nje ya chuo na hatua hiyo kupelekea idadi kubwa ya wanafunzi kuongezeka kujiunga chuoni hapa."Haya yote ni wajibu wetu kuwaelimisha wale wachache ambao bado hawajaelewa kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya CCM ili kuhakikisha wanatuchagua tena,"amesema Peter.

Mwenyekiti wa Seneti, Davis Peter amewaeleza hayo yote ni mambo ya kuwaeleza wazazi wote na vijana wenzao waliojiandikisha kuona umuhimu wa kuchagua CCM kwa kazi kubwa iliyofanywa chuoni hapo F.D.C kwa kipindi kifupi.

Katika kikao hicho kilichoudhuriwa na Makamu Mkuu wa Chuo,walimu,mlezi wa chuo na viongozi wa Serikali za wanafunzi, wote wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha Wilaya ya Sengerema madiwani wote wa CCM wanashinda na Mbunge Ndugu Tabasam anashinda kwa kishindo.

"Sambamba na hilo mkutano huo umeazimia kushirikiana vizuri na viongozi wetu wa Chama Cha Mapinduzi wa ngazi zote kumtafutia kura za kutosha mgombea wetu Dkt.John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha tunawapa zawadi ya kura za kutosha kutoka Wilaya ya Sengerema na majimbo yote ya Mkoa wa Mwanza yenye wagombea wa CCM,"amesema.



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news