Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mamlaka za Mitaa (TAMISEMI),Mwita Waitara wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Juma la Elimu yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Chemba mkoani Dodoma.
Waitara amesema kuwa, bila wananchi kutia nguvu katika baadhi ya maeneo, suala la kuboresha elimu kwa kila mtoto halitafikiwa badala yake kutaendelea kuwa na matabaka ya wenye uwezo na wasio na uwezo.
Ameeleza kwa kinachofanywa na Serikali ni kusaidia watoto wa masikini ambao hawakuwa na uwezo wa kusoma kutokana na kukosa ada hivyo ikaamua kuwekeza huko kwa kutoa fedha jambo lililosaidia ongezeko la uandikishaji watoto wanaoanza shule.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mamlaka za
Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara (kwanza kulia) akikagua moja ya
maabara iliyokarabatiwa katika Shule ya Sekondari Bihawana mkoani Dodoma.
Waitara akizungumza kuhusu chakula shuleni amesema kwamba, inawagawa wanafunzi kwa madai watoto wa masikini wanashindwa kusoma vizuri, kwani wanashinda njaa wakati wengine wanakula.
“Hatuwezi kufanya ushindani ukawa sawa kwa kila mmoja, elimu ni bure, sawa, lakini kuna watoto wanashinda wakipiga miayo wakati wenzao wamekula, katika hilo unawezaje kuwa na ushindani wa kweli, lazima wengine wawe juu na wengine wabaki chini,”amesisitiza Waitara.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mamlaka za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bihawana leo katika ziara yake ya kukagua shule kongwe zilizokarabatiwa nchini.
Baadhi ya walimu wa Shule Kongwe ya Bihawana wakimfuatilia kwa umakini Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mamlaka za Mitaa (TAMISEMI),Mwita Waitara ()hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao.
Awali kabla ya Uzinduzi wa Juma la Elimu, Waitara amekagua Shule ya Sekondari ya Bihawana kwani ni moja wapo ya kati ya shule kongwe 89 zilizopewa fedha kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Bihawana, Joseph Mbilinyi amesema kuwa, ukarabati katika shule hiyo umetumia kiasi cha shilingi 1,367,057.21 iliyotmika kukarabati maabara nne, matundu ya vyoo 32, mabweni nane, zahanati,msikiti, jengo la utawala, maktaba,bohari,mfumo mzima wa umeme, uchimbaji wa kisima cha maji, ukumbi wa mkutano, bwalo la chakula, ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na mabweni
Jengo la utawala la shule ya Sekondari Bihawana lililokarabatiwa hivi karibuni.
Muonekano wa moja ya maabara iliyokarabatiwa katika Shule ya Sekondari Bihawana mkoani Dodoma.
Pia katika shule kongwe zilizopokea fedha kwa ajili ya ukarabati na uboreshaji wa mindombinu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa ambapo pia ameridhishwa na ukarabati uliofanyika katika shule hizo na kuwataka wanafunzi hao kujitamba kwa kusoma kwa bidii na kupata ufaulu mzuri ili kuja kuwa viongozi na watendaji wa taifa.
Naye Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa, Annette Nara ameeleza kuwa elimu bila malipo imesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza na kidato cha kwanza, kupunguza kiasi kikubwa cha utoro wa wanafunzi kutokana na upatikanaji wa chakula shuleni kupitia Mpangowa EQUIP-T wa kuunganisha wazazi na walimu ili kusimamia mahudhurio ya wanafunzi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chembe walioshiriki Juma ya Elimu wilayani Chemba.
Muonekano wa moja ya jengo lililokarabatiwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa,
Mwalimu Mkuu wa Shule wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa, Flora Nussu amesema kuwa kiasi cha Shilingi 1,012,729,844.90 zimetumika katika ukarabati wa jengo la utawala, madarasa yote, mabweniyote, vyoo na bafu, bwalo la chakula , jiko na vifaa vya kupikia, maktaba, zahanati, miundombinu ya majisafi na maji taka, miundombinu ya umeme na mfumo wa TEHAMA, mfumo wa gesi katika maabara zote tatu, nyumba moja ya matroni.
“Ukarabati hu umeleta tija kubwa kitaaluma kwani ufaulu umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka hivyo tunakuhaidi kuitunza miundombinu hii ili kuendelea kufanya vizuri katika ufaulu wetu,”amesistiza Mwalimu Nussu.
Kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi Getruda Gabriel akiwasilisha kero waliyonayo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa leo wakati wa ziara ya Naibu waziri TAMISEMI alipotembelea shule hiyo kuona ukarabati uliofanykia katika shule hiyo.
Walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri TAMISEMI.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa wakimpokea Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika shule hiyo.
Katika Shule wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa, Getruda Gabriel kiongozi wa wanafunzi amepata nafasi ya kuwasemea wanafunzi wenzake kwa kueleza changamoto wanazo kutanana nazo kuwa ni uhaba wa maji usafiri wa shule kwamba kukitokea dharura hawana namna ya kusafirisha mgonjwa na kuomba kukarabatiwa barabara ya kufika shuleni hapo kwani miundombinu yake sio rafiki.Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com