Msemaji wa NATO, Oana Lungescu. Picha na NATO.
JUMUIYA ya Mkataba wa Kujihami (NATO) imeyapuuza madai ya Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko kwamba wanajiimarisha kijeshi katika eneo la karibu na mpaka wa Mashariki wa taifa hilo, Diramakini inakujuza zaidi..
NATO ambao ni ushirikiano wa kujihami ya kambi ya magharibi. Inaunganisha nchi 28 za Ulaya pamoja na Marekani na Canada huku ukiwa imeasisiwa Aprili 4, 1949 jijini Washington, D.C. Marekani
Oana Lungescu ambaye ni Msemaji wa jumuiya hiyo kutoka makao makuu yake mjini Brussels, Ubeligiji amesema kuwa,muungano huo wa kijeshi uwepo wa vikosi vya majeshi ya nchi wanachama katika upande huo wa Mashariki si kitisho kwa nchi yoyote na unalenga kulinda amani na kuzuia hali ya mizozo.
Awali, Rais Lukashenko alisema vifaru vya kijeshi na ndege za kivita za NATO vimepelekwa katika eneo hilo la umbali wa dakika 15 kutoka kwenye mpaka wa Belarus.
Aidha, NATO imesisitiza kuwa inafuatilia kwa karibu hali nchini Belarus na kuitaka nchi hiyo kuheshimu misingi ya uhuru, ikiwemo haki ya maandamano ya amani.
Serikali ya Belarus inakabiliwa na maandamano makubwa ya umma kuhusiana na matokeo ya uchaguzi wa rais ambayo upande wa upinzani unasema yalighubikwa na vitendo vya udanganyifu, hivyo kudai kutoridhishwa nayo.