TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza wagombea katika majimbo 18 wamepita bila kupingwa na watatangazwa katika gazeti la serikali, na kusisitiza inafanya kazi kwa kufuata sheria na Katiba ya Nchi na ni Tume huru.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume hiyo, Dkt.Wilson Mahera, ametangaza majimbo hayo ya waliopita bila kupingwa kupitia CCM jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.Amesema kuwa, waliopita bila kupingwa ni Elias Kwandikwa (Ushetu), Job Ndugai (Kongwa), Ahamed Shabiby (Gairo), Profesa Palamagamba Kabudi (Kilosa), Jonas Zeeland ( Mvomero), Kalogereris Shabani ( Mororgoro Kusini), Taletale Shabani (Morogoro Mashariki), Isaac Kamwelwe (Katavi).
Wengine ni Geofrey Pinda (Kavuu), Philipo Mulugo (Songwe), Zedi Jumanne (Bukene), Dkt. Hamisi Kigwangala (Nzega Vijijini), Kassim Majaliwa (Ruangwa), Nape Nnauye (Mtama), Vita Kawawa (Namtumbo), Jumanne Sagini (Butiama) Alexander Mnyeti (Misungwi) na January Makamba (Bumbuli).