MGOMBEA urais kupitia Chama cha Demokrasia Makini, Cecilia Augustiono Mwanga ameidhinishwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo kupitia Uchaguzi Mkuu Oktoba 28,mwaka huu.
Idhinisho Hilo limefanywa leo katika ofisi za makao makuu ya NEC jijini Dodoma na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage huku mgombea mwenza akiwa ni Tabu Mussa Juma.
Wengine walioidhinishwa ni pamoja na Yeremia Maganja wa NCCR Mageuzi na Mutamwega Mgaya wa SAU.
Hadi sasa walioidhinishwa ni vyama sita ikiwemo CCM ADA TADEA na NRA.
Kwa habari au matangazo (diramakini@gmail.com)www.diramakini.co.tz