NI YANGA SC, YAWACHARAZA AIGLE NOIR

LEO Agosti 30, 2020 ambayo ilikuwa Siku ya Mwananchi kupitia Yanga SC imekuwa ya furaha na shangwe kwa wananchi baada ya timu yao kuwapa burudani nzuri.

Ni baada ya Yanga SC kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa wa Burundi, Aigle Noir katika mchezo wa kirafiki uliomalizika punde katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Burudai hiyo ya aina yake ilishuhudiwa na maelfu ya mashabiki wa klabu hiyo ambapo pia ilikuwa ni kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ameshuhudia kandanda safi kati ya Yanga SC na Aigle Noir.

Warundi hao waliwaruhusu Yanga SC kupata mabao baada ya kiungo wake, Mghana Koffi Kouassi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 29 kufuatia kuonyeshwa kadi ya njano ya pili na refa Martin Sanya wa Morogoro.

Aidha, baada ya hatua hiyo, vijana wa Jangwani walipata bao la kwanza dakika ya 39 likifungwa na winga wake mpya, Tuisila Kisinda ambaye alimsoma vema mlinda mlango wa Aigle Noir, Erick Johola baada ya pasi nzuri ya Feisal Salum (Fei Toto).

Baadaye mshambulaji mpya ambaye ni Mghana Michael Sarpong aliifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 59 kwa kichwa kutoka umbali wa mita zaidi ya tano kufuatia 'cross' safi ya Ditram Nchimbi.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news