NSSF yatekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais Magufuli, wananchi wampa tano JPM

 
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu,Jenista Mhagama, amekiri utekelezwaji wa miradi ya kimkakati na maagizo mengine yaliyotolewa na Rais Dokta John Pombe Magufuli kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Diramakini inakujuza zaidi...

Amesema, Rais Dokta Magufuli alitoa maagizo mawili katika mradi wa nyumba za NSSF uliopo Dungu; kwamba wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni waingie katika nyumba hizo agizo ambalo limeshatekelezwa na nyumba 99 ambazo zimekamilika tayari zimepangishwa.

Jenista amesema hayo baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli ambapo alianzia ujenzi wa barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, na kuongeza kuwa NSSF inafanya kazi nzuri na ina uwezo mkubwa unaoweza kusaidia uwekezaji.

Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, Salimu Matimbwa, ambaye ni mmoja wa wapangaji wa nyumba za NSSF zilizopo Dungu amesema , amepata nyumba ambayo hakutegemea kama angeweza kupata kwa sababu ni nzuri, imejengwa kisasa na inastahili kuishi binadamu yoyote.

Mkazi wa Kigamboni, Felix John, aliishukuru Serikali kupitia NSSF kwa sababu imewasaidia vijana kupata ajira katika mradi huo wa ujenzi barabara inayounganisha Daraja la Nyerere.

Naye Godfrey Kurumwa ambaye ni dereva bodaboda ameipongeza Serikali pamoja na NSSF kwa kujenga barrabara pana ya kiwango cha lami.

Miongoni mwa wananchi hao wakielezea furaha yao kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli ambayo yamefanyiwa kazi kwa ufanisi na NSSF.

 Kwa uapnde wake, Meja mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Adiel Raphael Kaaya, amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi ambayo inaonekana dhahiri na kama kuna mtu ambaye ni mbishi aende akashuhudie ujenzi wa barabara hiyo ambayo ni nzuri na yenye ubora wa hali ya juu.

Mjasiriamali Mwajuma Salimu Shukuru ameishukuru Serikali na NSSF, kwa kukamilisha ujenzi wa kipande cha barabara inayounganisha Daraja la Nyerere, Kigamboni na kuainisha kuwa, kabla ya barabara hiyo ya lami walikuwa wanapata shida kubwa ya vumbi, hivyo kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua fursa za kiuchumi na kijamii.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio alimshukuru Rais Dokta Magufuli kwa sababu yanayofanyika ni matokeo ya maelekezo yake baada ya mkwamo wa muda mrefu wa kipande hicho cha barabara.

  Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news