RC Hapi awapongeza SAO HILL kwa kujenga bweni Shule ya Changalawe

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amewapongeza Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti la Sao Hill kwa kujenga bweni la Shule ya Sekondari ya Changalawe  iliyopo Mafinga Mjini katika wilayani ya Mufindi kwa kutumia zaidi ya shilingi milioni 114 na kuwaomba wadau wengi wajitolee kama ambavyo Sao Hill walivyofanya, anaripoti Fredy Mgunda kutoka Mufindi. 

Amesema hayo mara baada ya ukaguzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Changalawe wilayan Mufindi lililojengwa na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti Sao Hill.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka TFS na shamba la miti la Sao Hill, ambapo amewapongeza kwa kujenga bweni la Shule ya Sekondari ya Changalawe iliyopo Mafinga Mjini katika Wilaya ya Mufindi kwa kutumia zaidi ya shilingi milioni 114.

Katika risala ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Saada Mwaruka iliyosomwa na mkuu wa shule ya Sekondari  Changarawe imebainisha kuwa , ufadhili huo utasaidia jumla ya wanafunzi 80 kukaa shuleni hapo na kuondokana na hatari ya kukatisha masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la mimba kwa wanafunzi.

Alieleza namna jitihada zake za kuandika miradi ya utatuzi wa changamoto za shule ulivyosaidia kuwavutia wafadhili hao ambao Sao Hill hadi kufanikisha upatikanaji wa majengo kadhaa ikiwemo bweni hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akiwa na mkuu wa Shule ya Sekondari ya Changarawe wakati wa kukagua ujenzi wa bweni lilofadhiliwa na Sao Hill.

Hatua hii imeonesha kumpendeza Mkuu wa Mkoa, Ally hapi licha ya kuwataka viongozi wengine wa taasisi za serikali ikiwemo shule kujenga utamaduni wa kuandika miradi yenye kuomba ufadhili kwa wadau ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi.

Kando ya hayo awali katika ziara hiyo mkuu wa mkoa amefanya uzinduzi wa jengo la maabara katika Zahanati ya Rungemba wilayani humo na kuahidi kukabidhi mifuko 100 ya saruji ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za wananchi hao waliojitoa kuchangia na kukamilisha ujenzi wa maabara hiyo.

Maeneo mengine yalifikiwa na mkuu wa mkoa katika ziara hiyo iliyobatizwa jina la Iringa Mpya ni pamoja na Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Mafinga pamoja na eneo la ofisi za shamba la miti Sao Hill ambapo amepokea mtambo wa kisasa wa kuzimia moto ulionunuliwa na Serikali.


habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news