WANANCHI mkoani Mara wamepokea kwa furaha kuanza kutolewa kwa huduma za matibabu ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kwangwa Manispaa ya Musoma mkoani hapa.
Hospitali hiyo ilianza kujengwa tangu miaka ya 1977,i imekwama kumalizika na Serikali ya Awamu ya Tano kuinasua kwa kutoa shilingi Bilioni 15 kwa mkupuo ili kuikamilisha kutimiza dhamira ya Muasisi wa Hospitali hiyo Hayati Mwalimu Julius Nyerere, anaripoti AMOS LUFUNGULO.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akimjulia hali mmoja wa akinamama waliojifungua jana katika Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kwangwa Musoma.Mtoto huyo alipewa jina la Julius kama heshima ya kumuenzi Muasisi wa Hospitali hiyo Hayati Julius Nyerere ambapo huduma ya Mama na Mtoto zilianza kutolewa hapo jana. PICHA NA AMOS LUFUNGULO/www.diramakini.co.tzPamoja na kuanza kutolewa kwa huduma ya Mama na Mtoto jana pia huduma ya kusafisha figo inatarajia kuanza kutolewa hospitalininhapo na kufikia mwezi Oktoba,mwaka huu huduma za Hospitali ya Rufaa zitaanza kutolewa.
Sambamba na huduma za matibabu ya kibingwa ikiwemo upasuaji wa mifupa zitafuatia kwa baadaye ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Afya ya kusogeza huduma hizo kwa wananchi wake.
Neema Pius mkazi wa Kwangwa Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara ameieleza www.diramakini.co.tz kuwa, kutolewa kwa huduma ya mama na mtoto ni neema kubwa kwani kina mama watanufaika na elimu thabiti ya kutunza ujauzito na kujifungua salama jambo ambalo litaimarisha afya ya mama na mtoto pamoja na makuzi bora.
Naye Thabita Juma Mkazi wa Kiara amesema kuwa, kinamama wataondokana na usumbufu wa kufuata matibabu hayo mbali.
Amesema, watatumia muda mwingi kufanya shughuli za maendeleo tofauti na hapo awali, huku akimshukuru Rais Dkt.John Magufuli kwa kutoa fedha zilizopelekea kukamilisha ujenzi huo.
Kwa upande wake Ashura Pius mkazi wa Kwangwa amesema, kwa Sasa watapata huduma ikiwemo uzazi wa mpango pamoja na matibabu ya chanjo na kliniki kwa wajawazito wote kwa uhuru tofauti na awali huku akisisitiza watoa huduma kuendelea na moyo walionao wa kuwahudumia wananchi kwa upendo na kwa weledi wanapofika kutibiwa.
Pia Thobias Wambura mkazi wa Kwangwa aliyefika kushuhudia zoezi la kuanza kutolewa huduma hiyo emesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano imewatoa kimasomaso wakazi wa Mkoa wa Mara.Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara Dokt. Joachim Eyembe (kulia) akiwapa maelezo Mgombea Ubunge Jimbo la Musoma Mjini,Vedastus Mathayo( katikati) na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Mjini,Benedictor Magir walipofika kujionea kuanza kutolewa kwa huduma ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere hapo.PICHA NA AMOS LUFUNGULO/ www.diramakini.co.tz
Amesema,itakuwa ni mwarobaini wa kuokoa fedha nyingi ambazo awali wananchi walizitumia kufuata matibabu ya kibingwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, KCMC Moshi, pamoja na Bugando jijini Mwanza.
"Tusipoishukuru Serikali tutakuwa hatujaitendea haki hata kidogo, Rais Magufuli katatua kero kubwa ambayo wananchi wengi ikiwakumba, ilikuwa mtu akitaka kufanyiwa upasuaji wa mifupa lazima aende Bugando ama MOI, kwa sasa kitengo hiki kikianza kutatibiwa hapa hapa na gharama ambazo zingetumika kwenda huko zitafanya mambo mengine ya maendeleo kwa familia hakika Rais Magufuli katufanyia jambo jema lazima tumshukuru na kuzidi kumuombea kwa Mungu,"amesema Peter Matiku.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara,Dokt. Joachim Eyembe amesema kuwa,mpango uliopo kwa baadaye ni kuanzisha huduma za kubadilisha figo hospitalini hapo.
Amesema,kukamilika kwa hospitali hiyo ni fursa kiuchumi kwa wakazi wa Mkoa wa Mara kwani itapokea watu kutoka Mkoa wa Mara, Kanda ya Ziwa pamoja na nchi jirani ya Kenya na hivyo kuwa fursa ya utalii pia.
Dokt. Eyembe ametoa pongezi za dhati kwa Rais Magufuli, Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mara,Adam Malima kwa namna ambavyo wamefanikisha ujenzi huo ambao watu wengi walidhani usingekamikika kutokana na kukwama kwa miaka mingi iliyopita jambo ambalo amesema limewezekana kwa muda mfupi baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kulivalia njuga.
Mkuu wa Mkoa wa Mara,Adam Malima ambaye alikuwa mgeni rasmi katika zoezi hilo amema Rais Magufuli alichokifanya kwa wakazi wa Mara ni historia na heshima ya pekee ambayo kila mwananchi ataendelea kuikumbuka kwani fedha shilingi bilioni 15 alizotoa zimefanikisha ujenzi huo na kwamba waliodhani asingeweza kwa sasa wanashuhudia kwa macho yao mchana kweupe.
Kwa siku ya jana watoto watatu walizaliwa hospitalini hapo ambapo mtoto wa kiume alipewa jina la Julius kama ishara ya kukumbuka Muasisi wa ujenzi wa Hospitali hiyo Mwalimu Julius K.Nyerere, mwingine aliitwa Samia kama ishara ya kutambua mchango wa Makamu wa Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, na watatu aliitwa jina la Maria jina ambalo ni la mke wa Hayati Baba wa Taifa ,Mama Maria Nyerere.
Tags
Habari