Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya White Star Investment ya jijini Dar es Salaam inayofanya biashara za usafirishaji ndani na nje ya nchi kwa kutumia malori, Taalib Karim Mbowe anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma mbalimbali, Diramakini inakujuza zaidi...
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo,Afisa Uhusiano wa TAKUKURU, Doreen Kapwani amesema, taasisi hiyo inamshikilia mfanyabiashara huyo kwa makosa ya ukwepaji kodi,udanganyifu na utakatishaji wa fedha haramu.
"Pamoja na uchunguzi huu, TAKUKURU inachunguza umiliki wa vichwa vya malori zaidi ya 100 vinavyomilikiwa na mfanyabiashara huyo pamoja na mikopo yake ya zaidi ya dola za kimarekani milioni tatu (zaidi ya shilingi bilioni 6.3) kutoka Benki ya Barclays pamoja na dola za kimarekani 540,000 (sawa na shilingi bilioni 1.1) kutoka Benki ya Equity. Uchunguzi huu ukikamilika na kuthibitika tuhuma hizi, mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani,"amebainisha Kapwani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu.
Tags
Uchumi