SIKU chache baada ya Jamhuri ya Kenya kutangaza nchi 130 ambazo raia wataruhusiwa kuingia bila kukaa karantini na Tanzania kuwekwa kando katika orodha hiyo, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuchukua hatua.
Mkurugenzi wa TCAA, Hamza Johari amethibitisha hayo alipoulizwa na gazeti la Citizen.
Amedai,sababu za maamuzi ya kuondoa ruhusa kwa kampuni tatu za ndege za Kenya ni mgogoro unaoendelea kati ya nchi hizo.
Mataifa hayo yapo kwenye mvutano wa kutokukubaliana, ni juu ya Kenya inavyofanya kwa abiria kutoka Tanzania huku wao wakitaka kupewa kipaumbele.
Agosti Mosi, mwaka huu, TCAA ilipiga marufuku Shirika la Ndege la Kenya, Kenya Airways(KQ) kutua nchini, maamuzi ambayo TCAA ilisema ni kujibu Kenya kwa Tanzania kuondolewa kutoka kwenye nchi zenye ruhusa ya wageni wake kupokelewa Kenya bila kupitia vizuizi vya Corona.