UMOJA wa Falme za Kiarabu (UAE) umetoa amri ya kuibatilisha sheria ya kujitenga na Serikali ya Israel na kuruhusu sasa pande hizo mbili kuingia mikataba ya kibiashara na matumizi ya fedha.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari WAM, amri hiyo ya kiutendaji imetangazwa na Rais wa UAE,Mtukufu Sheikh bin Zayed Al Nahyan.
Uamuzi huo unalenga kuunga mkono ushirikiano wa pande mbili kwa ajili ya kuimarisha mahusiano yaliyoonyesha mwanga siku za karibuni.
Pia amri hiyo inakuja wakati Shirika la ndege la Israel, El Al likipanga kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya uwanja wa ndege wa Ben Gurion mjini Tel Aviv na mji mkuu wa UAE, Abu Dhabi.
Ndege hiyo itakuwa na ujumbe wa ngazi ya juu wa Israel na wasaidizi wa ngazi ya juu wa Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye alisimamia makubaliano ya kurudisha mahusiano kati ya pande hizo mapema mwezi huu.
Tags
Kimataifa