UEFA:Leipzig dhidi ya PSG nini nani zaidi nusu fainali leo?

BILA shaka fainali ya michuano mikubwa barani Ulaya imekuwa ya aina yake na yenye kusisimua. Kwa nini?, Ripota Wetu anakujuza...

Ligi ya Mabingwa kwa namna ya kipekee imetuletea matokeo ambayo hatukuyatarajia. Burudani, kuibuka kwa miamba mipya, matokeo ya kushtua, haya ni baadhi ya mambo yaliyojitokeza na tumeyashuhudia kwa siku kadhaa zilizopita.

 

Uhalisia ni kwamba, Juventus na Real Madrid waliishia katika nafasi ya robo fainali, ilitushangaza wengi. Huenda ukawa ni mwanzo tu, wa mengi tutakayo yashuhudia msimu huu.

 

Wataalamu Leipzig na wapambanaji Lyon wamefanikiwa kuweka historia kwenye hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. 

 

Upande wa pili, wakongwe Bayern Munich waliwachakaza Barcelona kwa magoli nane. Haipingiki, itawachukuwa muda Barcelona kupona maumivu haya.

Matokeo ya kushangaza kwenye hatua ya robo fainali yamepelekea kuwa na mpambano wa 

Kimataifa kati ya Ufaransa na Ujerumani kwenye hatua ya nusu fainali; Leipzig kuvaana na PSG,, Lyon dhidi ya Bayern Munich.

 

Usiku wa leo majira ya saa 4 tuna fursa ya kuangalia mtanange wa nusu fainali.Leipzig wameonesha umwamba wao kwa kuwaburuza Atletico Madrid kwenye hatua ya robo fainali katika mchezo uliokuwa na miujiza ya aina yake.

 

Siku moja kabla ya mchezo huo, ulionekana mtanange wa kusisimua kati ya PSG na Atalanta. 

 

Mwisho wa siku vijana kutoka Italia wakaambulia kipigo baada ya Wafaransa kupindua meza zikiwa zimesalia dakika tatu mpira kumaliza na kipenga cha mwisho kikalia wakati PSG akishinda kwa magoli 2-1.

 

Mpaka sasa, Leipzig na Paris Saint- Germain hawajakutana katika mchezo wowote, hii inapelekea kuwa na mchezo wa kuvutia Zaidi. 

 

Timu hizi ziliwahi kukutana mwaka 2014 katika mchezo wa kirafiki na Leipzig kuibuka na ushindi wa magoli 4-2.

Timu zote zimeweka historia ya kufika hatua ya nusu fainali. Tunaweza kusema hii ni mara ya pili kwa Leipzig kushiriki kwenye Ligi ya Mabingwa na wamefanikiwa kujiweka kwenye nafasi ya timu nne bora Ulaya kwa mara ya pili. 

 

Kwa maana hiyo, Leipzig wana kila sababu ya kusherehekea mafanikio haya kama watafika fainali au hata wakiikosa fainali.

 

Aidha, kwa upande wa mwingine, PSG  wanaendelea kulisogelea kombe la Ligi ya Mabigwa ambapo hawajawahi kushinda. 

 

Baada ya kubadilisha matokeo kwenye mchezo dhidi ya Atalanta, timu ya Tuchel wameonesha umwamba wao na fikra za kibingwa. PSG wana sababu ya kujiamini kwenye mchezo dhidi ya Leipzig.

   Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news