KUTOKA kwa Eric Shigongo, "Napenda nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufikia hatua hii leo. Mimi ni nani mpaka nistahili? Mungu ndiye anajua kusudi lake kwa watu wake, niwashuruku wajumbe kwa kuniamini na kunipigia kura nyingi.
Nawashukuru sana wana-Buchosa kwa maombi yenu, ndugu, jamaa na marafiki zangu kwa dua zenu. Tunayo kazi kubwa ya kuendelea kuombeana na kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindo, pia kuhakikisha Mhe. Magufuli anashinda miaka mitano tena na kufanya makubwa zaidi ya haya aliyofanya kwa miaka mitano iliyopita.
Nakishukuru sana chama changu CCM chini ya Mwenyekiti wetu, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuniamini na kunipa ridhaa hii ya kuipeperusha bendera ya CHAMA chetu katika Jimbo la Buchosa.
Nafahamu tulikuwa wengi kwenye mchakato, lakini chama chetu ambacho siku zote kimekuwa thabiti kimeona mimi ninafaa kukiwakilisha na kuwatumikia wananchi wa Buchosa.
Wananchi wa Buchosa, Chama changu na Taifa langu ninawaahidi sitawaangusha.... Tutapambana pamoja kuhakikisha ushindi na kuliletea maendeleo thabiti Taifa letu".
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI
Karibu! Tovuti hii ya www.diramakini.co.tz imesajiliwa rasmi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupewa leseni namba TCRA/OCS-BL/0197/2020 chini ya Diramakini Business Limited iliyosajiliwa nchini Tanzania kwa ajili ya kukuhabarisha, kukuelimisha na kukupasha habari mbalimbali toka ndani na nje ya nchi. Je? Una habari,maulizo au tangazo, unataka kutupa ufadhili? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com Asante.