"Ni miaka minne tangu tumepiga hii picha, na ndio siku ambayo tulipoanza kupanga mikakati ya kwenda kugombea Ubunge katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki kwa lengo la kuendelea kutoa mchango wetu katika Jamii.
Leo mwenzangu haupo ila najua uko ulipo unaona mumeo nimeshinda/ nimepita bila kupingwa nikimaanisha kwanzia leo mimi ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayesubiri kuapishwa tu na nipo tayari kwenda kumsaidia Mwenyekiti na Mgombea Urais wa CCM Mzee wangu John Pombe Magufuli kwenda kujaza kura zake nyingi za NDIO.
Mke wangu nitakukumbuka sana mke wangu, nitayaenzi yote tuliyokubaliana kufanya, nitakuwa Mbunge Mtumishi wa watu wote na sitoacha kuisimamia taasisi yako ya NASIMAMA NAO.
Nakupenda mke wangu ningefurahi tungelikuwa wote kusherekea nami ndoto yetu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ailaze roho yako mahala pema.