Umejiandaa kufika Dar es Salaam Oktoba? Utatumia usafiri wa mabasi, fuatilia taarifa usipotee

SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Joseph Magufuli imeendelea kutekeleza miradi kuanzia angani,baharini, nchi kavu na sasa Kituo cha Kimataifa cha Mabasi Mbezi Luis kipo mbioni kutumika, Diramakini imethibitisha...

Kituo hicho cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Mbezi Luis kimefikia asilimia 77 ya ujenzi wake na kinatarajiwa kuanza kazi rasmi ifikapo Oktoba, mwaka huu.
 
Afisa mmoja kutoka nchini Tanzania ameieleza Diramakini kuwa, kukamilika kwa kituo hicho ambacho kinatarajiwa kuwa cha kisasa pengine kuliko vituo vyote ndani na nje ya Afrika Mashariki kutaleta unafuu mkubwa kwa wasafiri.
"Kituo hiki kinaelekea kukamilika, kitakuwa cha kisasa zaidi pengine kuliko vingine ndani na nje ya Afrika Mashariki, haya ni matunda ya kodi za Watanzania, ndiyo maana sioni aibu kuwaambia watanzania waendelee kulipa kodi za Serikali kwa wakati, wachape kazi kwa bidii maana haya ni matokeo ya kodi zao,"Afisa huyo wa ngazi za juu ameidokeza tovuti hii ya Diramakini.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa kutoka Serikali ya Tanzania, ujenzi wa kituo hicho uliogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 50.9, utakapokamilika utakifanya kituo hicho kuwa moja ya kituo bora kati ya vituo vya mabasi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati huku kikitarajiwa kuchukua mabasi makubwa 108 kwa wakati mmoja.

 Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news