MKUU wa Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro,Mwangi Rajab Kundya amewataka waajiri mkoani humo kuwekeza kwenye masuala ya usalama na afya kwa wafanyakazi.
Mhandisi Ngata amesema, mafunzo hayo ambayo tayari yamefanyika katika mikoa ya Morogoro,Dodoma, Mwanza,Mbeya,Arusha na sasa Kilimnajaro, yatawasaidia waajiri kuweka mikakati madhubuti kwenye maeneo yao kazi, katika kupunguza au kuondosha ajali na magonjwa sehemu za kazi.
Afisa Mtendaji wa TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro, Boniface Mariki akizungumza kwenye mafunzo ya Vision Zero, mafunzo hayo maalumu yaliyoandaliwa na OSHA kwa kushirikiana na TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro yamefanyika Chuo cha VETA Moshi.
‘’Sambamba na mafunzo hayo, vile vile tunapata wasaha wa kusikiliza kero na changamoto zao, wakati wa utekelezaji wa Sheria na 5 ya mwaka 2003 ya Usalama na Afya, na kuzitatua,"amesema Ngata.
Naye Afisa Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara,Viwanda na Kilimo Nchini (TCCIA) Mkoa wa Kilimanjaro,Boniface Mariki anasema, mafunzo hayo yatawasaidia sana katika utendaji kazi wao, kwani wafanyakazi ni kiungo katika utekelezaji wa shughuli za viwandani, endapo mfanyakazi ataumia, itakuwa gharama kubwa kiuchumi, kwanza kumtibu na shughuli za uzalishaji zitaathirika.
Mariki amesema, wanachama wake wamefurahi kupata mafunzo hayo kwani Vision Zero ni mpya kwao, na hivyo wameahidi kutekeleza ipasavyo mkakati huo ambao umelenga kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi, na kuiomba OSHA kuendelea kuwapatia mafunzo kama hayo.
Afisa Mtendaji huyo wa TCCIA amesema, endapo waajiri watatenga bajeti zao za utakelezaji wa masuala ya usalama na afya kazi zitasaidia sana kuendeleza mipango yao na hivyo kuwa na uhakika wa uzalishaji.
Baadhi ya wanachama wa TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro wakisikiliza maada kwenye ufunguzi wa mafunzo ya Vision Zero, mafunzo hayo maalumu yaliyoandaliwa na OSHA kwa kushirikiana na TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro yaliyofanyika Chuo cha VETA Moshi.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tahimini toka toka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),Dkt. Abdulsalum Omari amesema, waajiri wanapaswa kufanya tathimini ya hali hatarishi sehemu zao kazi.
Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimnajro kwenye uzinduzi wa Mkakati wa Kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi, maarafu kama Vision Zero Mjini Moshi, Kundya amesema endapo waajiri watawekeza kwenye masuala ya usalama na afya, kwa kuweka mikakati endelevu ya kuwalinda wafanyakazi, wataweza kuongeza tija kwenye uzalishaji wao kwenye maeneo ya kazi.
Mgeni rasmi, Mwangi Rajabu Kundya Mkuu wa Wilaya ya Moshi (katikati) kwenye ufunguzi mafunzo maalamu ya Vision Zero mkoani Kilimanjaro amesisitiza ndapo waajiri watawekeza kwenye masuala ya usalama, uzalishaji utaongeza maradufu na mapato yataongezeka na hivyo kodi pia zitaongezeka hali itakayowezesha kuchangia kukuza uchumi wa taifa.
Aidha,kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa OSHA, Mkurugenzi wa Usalama na Afya Mhandisi, Alex Ngata amesema, mafunzo hayo yameandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwawezesha waajiri nchini kuhakikisha wanapunguza ama kuondosha kabisa ajali na magonjwa sehemu za kazi.
Mgeni rasmi, Mwangi Rajabu Kundya Mkuu wa Wilaya ya Moshi (katikati) kwenye ufunguzi mafunzo maalamu ya Vision Zero mkoani Kilimanjaro amesisitiza ndapo waajiri watawekeza kwenye masuala ya usalama, uzalishaji utaongeza maradufu na mapato yataongezeka na hivyo kodi pia zitaongezeka hali itakayowezesha kuchangia kukuza uchumi wa taifa.
Aidha,kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa OSHA, Mkurugenzi wa Usalama na Afya Mhandisi, Alex Ngata amesema, mafunzo hayo yameandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwawezesha waajiri nchini kuhakikisha wanapunguza ama kuondosha kabisa ajali na magonjwa sehemu za kazi.
Mhandisi Ngata amesema, mafunzo hayo ambayo tayari yamefanyika katika mikoa ya Morogoro,Dodoma, Mwanza,Mbeya,Arusha na sasa Kilimnajaro, yatawasaidia waajiri kuweka mikakati madhubuti kwenye maeneo yao kazi, katika kupunguza au kuondosha ajali na magonjwa sehemu za kazi.
Afisa Mtendaji wa TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro, Boniface Mariki akizungumza kwenye mafunzo ya Vision Zero, mafunzo hayo maalumu yaliyoandaliwa na OSHA kwa kushirikiana na TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro yamefanyika Chuo cha VETA Moshi.
‘’Sambamba na mafunzo hayo, vile vile tunapata wasaha wa kusikiliza kero na changamoto zao, wakati wa utekelezaji wa Sheria na 5 ya mwaka 2003 ya Usalama na Afya, na kuzitatua,"amesema Ngata.
Naye Afisa Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara,Viwanda na Kilimo Nchini (TCCIA) Mkoa wa Kilimanjaro,Boniface Mariki anasema, mafunzo hayo yatawasaidia sana katika utendaji kazi wao, kwani wafanyakazi ni kiungo katika utekelezaji wa shughuli za viwandani, endapo mfanyakazi ataumia, itakuwa gharama kubwa kiuchumi, kwanza kumtibu na shughuli za uzalishaji zitaathirika.
Mariki amesema, wanachama wake wamefurahi kupata mafunzo hayo kwani Vision Zero ni mpya kwao, na hivyo wameahidi kutekeleza ipasavyo mkakati huo ambao umelenga kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi, na kuiomba OSHA kuendelea kuwapatia mafunzo kama hayo.
Afisa Mtendaji huyo wa TCCIA amesema, endapo waajiri watatenga bajeti zao za utakelezaji wa masuala ya usalama na afya kazi zitasaidia sana kuendeleza mipango yao na hivyo kuwa na uhakika wa uzalishaji.
Baadhi ya wanachama wa TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro wakisikiliza maada kwenye ufunguzi wa mafunzo ya Vision Zero, mafunzo hayo maalumu yaliyoandaliwa na OSHA kwa kushirikiana na TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro yaliyofanyika Chuo cha VETA Moshi.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tahimini toka toka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF),Dkt. Abdulsalum Omari amesema, waajiri wanapaswa kufanya tathimini ya hali hatarishi sehemu zao kazi.
Amesema, waajiri wanatakiwa kutengeneza shabaha ili kutambua kuna ajali kiasi gani na magonjwa kiasi gani, ili waweze kuweka mifumo ya kudhibiti ajali na magonjwa sehemu za kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Sheria kutoka OSHA,Joyce Bupe Mwambungu amesema katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, wakala umelenga kujenga uelewa zaidi kwa wadau wake juu ya masuala mbalimbali ya usalama na afya ili kututua changamoto wakati wa utekelezaji wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi.
Mwambungu amesema, yapo maboresho mengi ambayo OSHA imeyafanya na inaedelea kuyafanya ili kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara kwa wadau, na mpaka sasa tozo na ada mbalimbali zilizokuwa zikitozwa zimeondolewa ili kurahisisha utekelezaji wa sheria.
Pia Mwambungu amesema, kwa mwaka huu wa fedha kupitia bajeti iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango wameondoa Tozo ya Elimu kwa Umma, ambayo ilikuwa ikitozwa, hivyo sasa ni fursa kwa waajiri kuwasiliana na OSHA kwa kumwandikia Mtedaji Mkuu.
‘’Tozo za mafunzo zipo kisheria zinabaki kama ilivyo, ila tozo ya Elimu kwa Umma ndio imefutwa, hivyo waajiri watapatiwa elimu hiyo bure ambayo ilikuwa ikitozwa endapo OSHA itakuja kukupatia elimu,"amesema Mwambungu.
Mafunzo ya Vision Zero mkoani Kilimanjaro yameandaliwa na OSHA kwa kushirikiana na TCCIA mkoani humo kwa lengo la kuitambulisha Vision Zero kwa waajiri na wanachama wa TCCIA.