Wanajeshi wamtangaza Kanali Goita kuwa Rais kimya kimya

KANALI Assimi Goita ambaye ni kiongozi wa wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Mali hivi karibuni ameteuliwa na jeshi hilo kuwa Rais wa mpito.

Uamuzi huo unafikiwa ikiwa zimepita siku zaidi ya 10, baada ya wanajeshi hao kumuondoa madarakani, Rais Ibrahim Boubacar Keita.

Kwa mujibu wa tarifa kutoka mjini Bamako, Mali inadaiwa wanajeshi waliofanya hao wamemchagua kiongozi wao Assimi Goita kuwa Rais kwa ajili ya kuongoza kipindi cha mpito.

Aidha,kabla ya hatua hiyo, Kanali Assimi alikuwa kiongozi wa Kamati ya Taifa ya Kijeshi (CNSP) iliyoundwa baada ya kuondolewa madarakani Rais Keita.

Wakati hayo yakijiri, tayari Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) imewataka viongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Mali kukabidhi madaraka kwa serikali ya mpito ya kiraia mara moja na waitishe uchaguzi ndani ya kipindi cha mwaka mmoja ujao.Jeshi linataka kuongoza miaka mitatu 


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news