TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita imekabidhi shilingi milioni 38.4 kwa Chama cha Ushirika cha Kuweka na Kukopa cha Wafanyabiashara wa Geita (Geita SACCOS) ambazo zimeokolewa kutoka kwa wadaiwa sugu 11 ambao walikuwa wamekopeshwa na chama hicho na kukwepa kulipa madeni yao,anaripoti Robert Kalokola kutoka Geita.
Leonidas Felix, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo kwa Mhasibu wa Geita SACCOS, Angela Mabula amesema, taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa fedha hizo ambazo wanachama walikuwa wamekopeshwa kijinai kwa sababu wakati wa kukopeshwa hawakuwa na sifa na vigezo vya kukopeshwa.Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita, Leonidas Felix (kulia) akikabidhi fedha
shilingi milioni 38,486,600 kwa Angela Mabula, Mweka hazina wa Geita SACCOS zilizorejeshwa na wadaiwa sugu baada ya kubanwa na taasisi hiyo.Picha na
Robert Kalokola-Diramakini.
Amesema kuwa ,
fedha hizo ni sehemu ya zaidi ya shilingi milioni 400 ambazo Geita SACCOS inadai
kwa wanachama ambao wameshinda kurejesha kwa hiari yao.
Felix ameongeza kuwa, baada ya TAKUKURU kuwabana wadaiwa sugu wote na kuwataka
kurejesha kwa hiari yao kwa muda Maalum walioitikia ni 11 na
kurejea kiasi hicho.
Amesema
kuwa, uchunguzi wa sakata hilo ulitokana na ripoti ya ukaguzi ya vyama
vya ushirika iliyofanywa na COASCO iliyokabidhiwa kwa Waziri wa Kilimo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Japhet Hasunga .
Felix
ameeleza kuwa, ripoti ya COASCO ilibaini wadaiwa sugu kuwa na deni la
shilingi milioni 26, lakini TAKUKURU baada ya kufanya uchunguzi ilibaini kuwepo
kwa deni la wadaiwa sugu zaidi ya shilingi milioni 400.
Amesema,
fedha hizo zilizorejeshwa shilingi milioni 38.4 na baada ya uchambazi imebainika
kuwa shilingi milioni 31,391,293 ni za NSSF ,6,685,244.45 ni za TIB na 410,000 ni za
benki ya CRDB.
Amesema, hatua inayofuata kwa wale
ambao hawakutii amri halali ya kutakiwa kurejesha fedha hizo za
ushirika,ni kuwachukulia hatua za kijinai.
Amesema
kuwa, katika uchunguzi huo taasisi hiyo imekumbana na chamgamoto ya
baadhi ya wanachama kupewa mikopo bila kukidhi vigezo,baadhi ya kuwa nje
ya nchi pamoja na wadhamini wao,baadhi ya wanachi wenye madeni kuwa na
hali mbaya kiuchumi.
Amesema
kuwa, TAKUKURU imefuatilia madeni ya wadaiwa wakubwa wanachama 27 na
madeni madogo wanachama 235 na uchunguzi unakamilishwa ili kufikishwa mahakamani.
Mhasibu wa
Geita SACCOS Angela Mabula amesema kuwa, TAKUKURU imesaidia kung'ata na
kuwarejeshea shilingi milioni 38.4 ambazo ushirika huo ulizipata kutoka NSSF,TIB
na CRDB na kuwakopesha wanachama wao.
Amesema
Geita SACCOS ilikuwa imetumia madalali wa kawaida kukusanya madeni hayo,
lakini walikuwa wakilipwa asilimia 10 yao wanaondoka bila kufanya kazi
hiyo kwa ufanisi mzuri.
Kaboja
Jafari, Mhasibu wa NSSF amesema kuwa, mfuko huo wa hifadhi ya jamii
ulitoa mikopo kwa wanachama wake kupitia Geita SACCOS kati ya mwaka 2012,
lakini walishindwa kurejesha na kusababisha hasara.
Amesema, TAKUKURU wameweza kusaidia kurejesha zaidi ya sh.milioni 31 za mfuko huo
hivyo kuomba Serikali kuendelea kuimarisha taasisi hiyo ili iendelee
kusaidia.
Je, una habari,maulizo au tangazo? Tuwasiliane; diramakini@gmail.com
Tags
Uchumi