ZAIDI ya waumini 1000 wa taasisi ya kidini inayojulikana kama Shincheonji Church of Jesus jana wameshiriki kuchangia utegili (blood plasma ) kwa ajili ya kusaidia kutengeneza tiba ya virusi vya Corona (Covid-19).Hili limefanyika kutokana na wito wa mamlaka ya afya nchini Korea Kusini, Agosti 24, mwaka huu kuliomba Kanisa la Shincheonji kuchangia utegili kwa ajili ya utengenezaji wa tiba.
Mapema mwaka huu takribani visa 5000 vilipatikana kwa waumini wa Kanisa la Shincheonji, ambayo ni maambukizi makubwa zaidi kwenye jiji la Daegu, ila wengi wao wamepona virusi hivyo na watu 11 kufariki.
Kutokana na taarifa kutoka Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Magonjwa nchini Korea Kusini (KCDC), waumini 562 waliopona walifanikisha kuchangia utegili (blood plasma) na waumini 409 wamechangia utegili mwezi Julai, mwaka huu kupitia ushirikiano na KCDC na Kanisa la Shincheonji
Kutokana na mahitaji ya uwezeshaji wa utengenezaji wa kinga, kutokana na utegili na majaribio ya mahabara, KCDC waliomba tena waumini wa Kanisa la Shincheonji kuchangia kwa wingi utegili mwezi huu, KCDC kwenye taarifa yao rasmi imelipongeza Kanisa la Shincheonji (Mwenyekiti Lee Man Hee) kwa kushiriki kikamilifu kwenye ukusanyaji wa utegili kama kikundi kwa ajili ya utengenezaji wa tiba kwa ajili ya usalama wa taifa na Dunia kiujumla, kwenye kipindi hiki cha majanga yanayosabishwa na Covid-19.Kwa kushirikiana na jiji la Daegu, na Chama cha Riadha jijjini Daegu, walipanga kutoa vifaa na wafanyakazi kwa ajili ya uchangiaji wa damu kuanzia jana hadi Septemba 4, 2020.
“Tunatoa shukrani zetu kwa jiji kwa kutoa sehemu za kuchangia damu kimakundi. Na pia tunatoa shukrani zetu kwa waumini wa Kanisa la Shincheonji,”amesema Kwon jun-wook ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa KCDC.
Tafiti na utengenezaji wa tiba kwa kutumia utegili unaendelea na Serikali kwa kushirikiana na Green Cross (CG) Dharma, ambayo ni kampuni ya Bioteknolojia nchini Korea kusini .
Wakati huo huo, Shirika la Chakula na Madawa la Marekani (FDA) limeidhinisha matumizi ya dharura ya utegili (Plasma) kwa matibabu ya Covid-19. Watalamu wanasema, kuna uhitaji wa kukusanya wa taarifa nyingi kwa ajili ya faida ya matibabu hayo.
Changamoto kubwa ya utafiti wa ufanisi na utengenezaji wa tiba hii ya utegili inakuja kutokana na uchache wa wachangiaji ambao wamepona virusi vya corona.Kama kiongozi wa dini, mnamo mwezi Julai mwaka huu, Mwenyekiti wa Kanisa la Shincheonji, Lee man Hee alisema “hii (uchangiaji wa utegili) ni kazi ambayo inatakiwa ifanywe na wananchi na waumini wa kweli. Nikushika amri ya Yesu ya kumpenda jirani yako kama nafsi yako(Math 22:39) ya kwenye Biblia," anasema Kiongozi huyo, www.diramakini.co.tz