WAZIRI UMMY MWALIMU:TUENDELEE KULIOMBEA TAIFA LETU, SERIKALI INAWATHAMINI SANA

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu amewataka viongozi wa dini kote nchini kuendelea kuliombea Taifa amani, umoja na mshikamano kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu.

Rai hiyo ameitoa leo wakati akiongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mtakatifu Agustino wa Hippo Chumbageni Tanga.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kushoto akipokea mchango kutoka kwa Catherine Kitandula wakati wa harambee hiyo.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati alipoongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mtakatifu Augustino wa Hippo Chumbageni Tanga, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Canon Rev Chistopher Kiango ambaye ni Kasisi Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga.

Katika harambee hiyo walifanikiwa kukusanya fedha taslimu shilingi milioni 13.7 papo hapo na ahadi ikiwa ni milioni 47.2 huku mwisho wa kukusanya michango hiyo ikiwa ni Septemba 20, mwaka huu.

Katika harambee hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa na viongozi wa dini wakiwemo waumini huku kwaya mbalimbali zikitumbuiza.

“Lakini pia tunawashukuru viongozi wa dini kwa jinsi walivyotuunga mkono kwa sala za kila siku katika mapambano dhidi ya Corona na Mungu akatuepusha na janga hili,hivyo niwaombe hata wakati huu nchi ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu tuendelee kuiombea nchi,”amesema Waziri Ummy.

Canon Rev Chistopher Kiango ambaye ni Kasisi kiongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga akizungumza wakati wa harambee hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa halfa hiyo.


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kushoto akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa Katibu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Tanga Mtaa wa Mt.Augustino wa Hippo Chumbageni Tanga.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kushoto
akipokea mchango wa mtoto Nicolaus Galula wakati wa harambee hiyo.
Meneja wa Hoteli ya Tanga Beach ya jijini Tanga, Joseph Ngoyo akizungumza jambo wakati wa harambee mara baada ya kukabidhi mchango wake kwa niaba ya familia yake. Kwaya ikitumbuiza wakati wa harambee hiyo.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa dini na Serikali baada ya kufanikisha harambee hiyo.

“Nimekuwa nikipata ujumbe kutoka kwa mawaziri wa nchi nyingine Afrika wakitaka kujua tumefanya kitu gani mpaka hakuna Corona, niseme kwamba ugonjwa huo umetoweka kutokana na Mungu ameipenda Tanzania,”amesema Waziri Ummy.

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi Katibu wa kanisa hilo, Cyprian Mtweve amesema, lengo la harambee ya leo katika kuadhimisha sikukuu ya Mt.Agustino wa Hippo ni kupata kiasi cha sh.milioni 125 kwa ajili ya kuezeka kanisa.

Mteve amesema, wanaamini kiasi hicho sio kikubwa kwa Mungu cha kushindwa kupatikana huku wakimshukuru mgeni rasmi kuwaongozea zoezi la harambee hiyo na kushiriki kwa moyo na kwa ukamilifu.

Amesema, upanuzi wa jengo la kanisa hilo umekuwa ukifanywa kwa kulirefusha kwa kiwango ambacho mawasiliano baina ya kasisi anayeongoza ibada madhabahuni na waumini wanaokaa viti vya mwishoni nyuma ya kanisa yanakuwa hafifu sababu ya umbali.

“Jengo hili limejengwa kwa kutumia teknologia ya zamani isiyohimili uwekwaji wa mifumo mbalimbali ya kisasa ikiwemo ile itakayoboresha ibada,"amesema.

Miongoni mwa viongozi ambao wamechangia kwenye harambee hiyo ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Profesa Palamagamba Kabudi wakiwemo wakuu wa wilaya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news