JUMUIYA ya Walinganiaji Dini ya Kiislam Duniani (World Islamic Call Society) imesema itaendelea na mpango wake wa
kusaidia makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo walemavu, vikongwe pamoja
na maskini wasiojiweza nchini Tanzania, anaripoti FATMA ALLY,www.diramakini.co.tz
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa jumuiya hiyo Tanzania, Ahmad Mus hab
Almajlubu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo
amesema jumuiya hiyo kwa sasa imerudi rasmi.
Amesema
kuwa, jumuiya hiyo imejikita zaidi katika kusaidia watu mbalimbali
wenye uhitaji maalum ambao wamekuwa na maisha duni kwa kuwachimbia visima
vya maji safi na salama, kujenga nyumba za ibada, madarasa pamoja na
kutoa elimu ya lugha ya Kiarabu.
"Jumuiya hii imeanzishwa mwaka 1984 na makao makuu yake yanapatikana
mjini Tripol nchini Libya ambapo imejikita zaidi kuisaidia jamii katika
kuwaendeleza kielimu kwa kutoa elimu ya ufundi (kushona) pamoja na
kompyuta,"amesema Ahmad.
Aidha,
amesema mbali na kutoa misadaa hiyo, lakini pia imekuwa na utaratibu wa
kuwapeleka nje wanafunzi bure waliomaliza kidato cha nne na sita kwa
lengo la kujiendeleza na elimu ya juu ili kujikwamua kimaisha.
Ameongeza
kuwa, mpaka sasa wametoa misaada ya kuchimba visima, kutoa vifaa vya
walemavu, kujenga misikiti katika mikoa ya Dar es Salaam,Dodoma pamoja
na Zanzibar.
"Licha ya
mikoa hiyo, lakini pia tumekuwa na utaratibu wa kufururisha katika mikoa
mingine pamoja na kutoa vifaa mbalimbali vya shule na madrasa sambamba
kuitafsiri Quran kwa lugha mbalimbali ikiwemo Kiswahili,"amesema Ahmad.
Tags
Habari