CHAMA cha ACT Wazalendo kimesema iwapo Watanzania watakipatia
ridhaa ya kuwaongoza kuanzia Oktoba 28, mwaka huu kwa nafasi za udiwani,
uwakilishi, ubunge na urais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kitaenda kuboresha maisha yao, kwani Kazi na Bata inawezekana.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo,Zitto Kabwe akimnadi mgombea Ubunge wa Kilwa Kaskazini Shaweji Mketo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa Kipatimu.
Mbali na hayo Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kwamba, iwapo atateuliwa na wananchi kuwa rais wa Zanzibar atahakikisha anaweka mfumo mpya wa uongozi ambao utajali na kuwaheshimu wananchi kwa mujibu wa Katiba.Taarifa mpya bonyeza hapa.
Amesema mfumo huo mpya ambao utaongoza serikali kwa kuzigatia haki na fursa sawa kwa wananchi wote bila ya kujali itkadi yake ya kisiasa.
Maalim ameyaeleza hayo leo katika kongamano la vijana wa Chama cha ACT-Wazalendo ambalo limeandaliwa na Ngome ya Vijana ya chama hicho na kuwashirikisha vijana kutoka mikoa yote ya Unguja, ambapo limefanyika katika Ukumbi wa S5 uliopo Kiembesamaki jijini Zanzibar.
Amesema, endapo mchakato utakamilika na kuchaguliwa na wananchi wa Zanzibar kuwa rais anakusudia kuanzisha mfumo mpya wa serikali ambao ataongoza kwa kujali na kwaheshu wa wananchi wa mujibu wa katiba ya nchi.
Maalim amesema,mfumo huo utakaoongoza nchi utaheshimu na kuzingatia haki zote za binadamu ambapo kila mwananchi atapata fursa na haki sawa bila ya kujali dini na itikad yake ya siasa.
"Waheshimiwa Mungu akijalia mkanchagua nitahakikisha kwamba tunaweka mfumo mpya wa uongozi na kila Mzanzibar atanufaika na kushi vizuri," amesema Maalim.
Wakati huo huo, mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Shinyanga Mjini, Godwin Makomba amewataka wananchi wa jimbo hilo kubadilika kwa kuwachagua wagombea wanaotokana chama hicho kuanzia udiwani, ubunge na urais iwapo wanahitaji maendeleo ya kweli na ya haraka.
Ameyasema hayo katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho ambao umefanyika katika eneo la viwanja vya Soko Kuu mjini Shinyanga.
Mgombea huyo amesema, kuendelea kuwachagua wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wataendelea kupewa ahadi zisizotekelezeka kila wakati
Amesema, huu ni wakati wa kuchagua mtu mwenye maono ya mbali katika kuwaletea maendeleo na mwenye uchungu na jimbo lao tofauti na wagombea wa CCM.