Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Lilian Mpanju Rugaitika akizungumza na mwananchi wakati alipotembelea banda la TIA maonesho ya Vyuo Vikuu yanayofanyika jijini Dar es Salaam, Mpanju amesema maonesho hayo yamesaidia kusogeza huduma kwa wanafunzi na kupata taarifa mbalimbali na baadhi ya wanafunzi wamepata udahili moja kwa moja katika banda hilo.
Mwakilishi wa Wanafunzi waTaasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Said Majujuka akiwapa uzoefu wa wanafunzi wa kujiunga na taasisi hiyo kutokana mikakati ya ufundishaji iliyopo katika taasisi hiyo, wakati wanafunzi hao walipotembelea Banda la TIA katika Maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkutubi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Magreth Mwamaso akizungumza na mwanafunzi aliyetembelea banda la TIA maonesho ya vyuo vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkutubi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), France Mwambene akitoa maelezo kwa wanafunzi wakati walipotembelea banda la TIA katika maonesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakifanyiwa udahili katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania katika Maonesho ya Vyuo Vikuu jijini Dar es Salaam.
Makamu wakuu wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Dkt. Matei Mapunda akitoa maelezo kwa wafanyakazi wanaotoa huduma katika maonesho ya Vyuo Vikuu viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo-Taaluma, Ushauri na Utafiti wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Dkt.Momole Kasambala (mwenye suti) akizungumza kuhusiana na maonesho ya vyuo vikuu yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, katikati ni Makamu wa Chuo- Fedha na Utawala, Dkt.Matei Mapunda kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma, Lilian Mpanju.
Tags
Picha