BARBARA GONZALEZ:SIMBA SC SASA NI ZAIDI YA MAKOMBE TU

"Ninahaidi makubwa Simba SC, ikiwa ni pamoja ya kutetea makombe yote tuliyochukuwa msimu uliopita, kikubwa ushirikiano wa wanachama, mashabiki na wadau wote wa Simba kwa ujumla;

Barbara Gonzalez ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Simba SC na anayerithi mikoba ya aliyekuwa katika nafasi hiyo, Senzo Mbatha Mazingisa aliyetimkia Yanga SC hivi karibuni ameyasema hayo muda mfupi baada ya kutambulishwa na Bodi ya Wakurugenzi klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Mohammed Dewji.

 "Tangu kuondoka Senzo Mbatha ni mwezi sasa, nimeshika nafasi kwa kukaimu kama Afisa Mtendaji Mkuu, kwa kweli tumepambana.Nipo hapa kuendeleza vision (maono) ya Simba SC kwa upande wa menejimenti, mimi nimenyooka na tutanyooka mbele, tumejipanga kwa ufupi ili kufikia malengo,"amesema.

Awali, Mohamed Dewji amesema kuwa, sio yeye peke amemteua Barbara Gonzalez kushika nafasi hiyo, bali Mkutano wa Wajumbe wa Bodi ndio umempendeza baada ya kukaimu nafasi hiyo tangu kuachwa na Senzo. 

Pia Dewji amemkaribisha Barbara na kumweleza kuwa mvumilivu kutokana na mambo mbalimbali ambayo ni mazuri na mengine ya ovyo ambayo wakati mwingine ni changamoto.

Maboresho hayo makubwa yanaendelea katika klabu hiyo ambapo pia jana walifanya maamuzi mengine kama inavyoonekana hapa chini.



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news