Bernard Membe:Mkituchagua ACT Wazalendo tunaenda kuyatekeleza haya kikamilifu

MGOMBEA Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo, Bernard  Membe amesema,ikiwa Watanzania watampa ridhaa mwaka huu, Serikali atakayoiongoza italetea neema kubwa.

Membe ameyasema hayo katika mwendelezo wa kampeni za chama hicho mkoani Lindi.

 "Mkituchagua, tutahakikisha hadi mwaka 2025 asilimia 60 ya watu wote wanaojihusisha na shughuli za kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara ndogo zilizosajiliwa wamekuwa na hifadhi ya jamii na wananchi wote kuwa na bima ya afya.

“Tutasimamia upatikanaji wa maisha stahiki ya uzeeni kwa kuwa na mfumo madhubuti wa Hifadhi ya Jamii ambao utahakikisha kuwa kila Mtanzania anakuwa na Bima ya Afya na Pensheni akifika umri wa kutoweza kufanya kazi.
“Tutahakikisha elimu ya Afya inawafikia Watanzania wote ili wawe na uwezo wa kulinda afya zao na kujiepusha na maradhi yanayoambukiza na yasiyoambukiza, hasa yanayotokana na mfumo wa maisha na majeraha,"amesema.

Pia amesema, wataunda mfumo wa huduma za afya kwa kuzingatia misingi ya usawa na ushirikishwaji wa jamii katika kufanya maamuzi yanayohusu masuala hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news