BREAKING NEWS: Baba aua binti yake, mwingine mbaroni kwa kubandua bango la mgombea

ANTHONY Costantine  (50) mkazi wa Kijiji cha Iseni anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kumuua binti yake Veronica Anthony (17) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kayenze.

Wakati huo huo,mkulima na mkazi mmoja wa Kijiji cha Mwabuki wilayani Misungwi  aliyefahamika kwa jina moja la Anthony anashikiliwa na jeshi hilo akidaiwa kubandua kwa makusudi bango lenye picha ya mgombea ubunge Jimbo la Kwimba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro ameyathibitisha hayo wakati akizungumzia kuhusiana na hatua ya kuwashikilia watu watatu kutokana na makosa mbalimbali ya uhalifu na mauaji.

Akizungumzia juu ya mauaji hayo,Kamanda Muliro amesema,mwanafunzi huyo aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito  kichwani na baba yake mzazi  Septemba 8, mwaka huu, majira ya saa nne usiku katika Kijiji cha Iseni,Kata ya Kayenze iliyopo Manispaa ya Ilemela,baada ya kuchelewa kurudi nyumbani.

Muliro amesema,kitendo hicho cha binti huyo kuchelewa kurudi nyumbani kilimuudhi na kumkasirisha baba yake na kuamua kutoa adhabu hiyo ya kikatili kwa binti yake na kusababisha kifo chake.

"Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wazazi, walezi na familia kwa ujumla kuwa makini na adhabu wanazotoa kwa watoto kwani zinaweza kusababisha kutenda ukatili dhidi ya watoto na kuleta madhara makubwa kwenye familia na baadaye kufikishwa mahakamani kwa makosa ya jinai,”amesema Kamanda Muliro.Kwa habari mpya soma hapa.

Aidha, akizungumzia tukio la pili Kamanda Muliro amesema, Mussa Gabriel maarufu kama Majuto mwenye umri wa miaka 35 anadaiwa kumuua Emmanuel Joseph (49) kwa kumpiga na kitu kizito utosini na kufariki papo hapo tukio lilitokea Septemba 9, mwaka huu, majira ya saa 7:00 huko Mhonze “A”, Kata ya Shibula iliyopo Manispaa ya Ilemela.

Amesema,chanzo kilidaiwa kuwa marehemu alikuwa akimtuhumu Majuto kumwibia simu ya mkononi aina yaTecno yenye thamani ya sh.40,000 fedha za Kitanzania.

Muliro amesema kuwa, miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali za Rufaa ya Kanda Bugando (BMC) na ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure kwa auchunguzi mara upelelezi utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Wakati huo huo, Kamanda Muliro amesema, mkulima na mkazi mmoja wa Kijiji cha Mwabuki wilayani Misungwi  aliyefahamika kwa jina moja la Anthony anashikiliwa na jeshi la polisi akidaiwa kubandua kwa makusudi bango lenye picha ya mgombea ubunge Jimbo la Kwimba.

Kamanda Muliro ameeleza kuwa, mtuhumiwa huyo alibandua bango lenye picha ya Shanifu Mansoor ambaye ni mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, kitendo kinachokiuka sheria za uchaguzi, tukio lililotokea Septemba 9, mwaka huu, majira ya 1:00 jioni,katika Kijiji cha Nyamilama wilayani Kwimba ambapo atafikishwa mahakamani haraka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news