Kwa nini Membe amesema hivyo?
Awali kabla ya taarifa zote za kumtangaza Lissu na baadae Membe kuzibatilisha taarifa hizo, Diramakini ilimnukuu Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad wakati akimnadi mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrsia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu katika mkutano wake wa kampeni akieleza kuwa ana imani Lissu atakuwa Rais wa Tanzania.
Maalim Seif ameyaeleza hayo katika Uwanja wa Mpira wa Mwanakombo katika Jimbo la Mohonda Wilaya ya Kaskazini B Unguja katika mfululuzo wa kampeni zake visiwani humo.
Amesema hana wasiwasi kuwa, Lissu atakuwa Rais na amesema akiingia madarakani mgombea huyo wa CHADEMA na yeye akiwa Rais wa Zanzibar siku ya pili tu baada ya kuapishwa atamtaka amkabidhi Mashekhe wa Zanzibar ambao wamewekwa ndani Tanzania Bara.
“Imani yangu Lissu atakuwa Rais wa Tanzania na mimi nitakuwa wa Zanzibar itakuwa raihisi Mashekhe wetu kuwarejesha,"ameeleza Maalim Seif. "Lakini ikitokea bahati mbaya akirudi huyo Magufuli na mimi nikiwa Rais nitamtumia ndege, lazima awatowe watu wangu,”amesema. Aidha, baadae Maalim Seif ambaye ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa alimthibitisha rasmi Lissu kuwa ndiye mgombea ambaye watamuunga mkono.