Gari analotumia Salum Mwalimu ambaye ni Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA limepata ajali eneo la Msoka Kata ya Ngogwa wakati wakiwa njiani kutoka kwenye mkutano Kahama. Wote waliokuwa kwenye gari hilo wametoka salama, taarifa ya CHADEMA imebainisha.Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema gari alilokuwa anatumia Mgombea Mwenza wa Urais CHADEMA imepata ajali na wote waliokuwa kwenye gari hiyo ni wazima wa afya.
“Tunamshukuru Mungu kwa kuwaponya katika ajali hii mbaya wote waliokuwa kwenye gari hii inayotumiwa na mgombea wa kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Salum Mwalimu Juma Mwalimu,"Tumaini Makene ameeleza.