Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera Charles leo Septemba 04, 2020 ameongoza kikao cha Maridhiano kati ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu ushiriki wa TBC katika kuripoti kampeni za uchaguzi mkuu kwa wagombea wa CHADEMA. Kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam, kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile.
Tags
Siasa