MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Karatu mkoani Arusha,Daniel Awaki amewahidi wananchi wa jimbo hilo waliopo katika Kata ya Mang'ola kuwajengea shule ya bweni ya wasichana ili kupunguza tatizo la mimba na kupandisha viwango vya ufaulu.
Awaki ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo uliofanyika katika kiwanja cha Mang'ola Barazani uliopo katika kata hiyo, ambapo amefafanua kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakishindwa kuendelea na masomo kutokana na kupata mimba kipindi wakiwa shuleni.
"Kumekuwa na tatizo la mabinti wetu kupata mimba wakiwa shuleni na hii inatokana na vishawishi wanavyovipata huko njiani wakati wakielekea shuleni, sasa nawaahaidi mkinipa kura zenu nitahakikisha najenga shule ya wasichana ya bweni ambayo itasaidia kupunguza tatizo hili kwani wanafunzi watakuwa wanakaa shuleni namaanisha katika mabweni, hivyo itasaidia kuepuka vishawishi ambavyo wanapata wakiwa njiani,"amesema.
Pa amewahidi wananchi wa jimbo hilo kuwawekea wakili ambaye atakuwa anawasaidia katika kesi zao ili wasiweze kuzudhulumiwa katika kesi zao mbalimbali,ambapo pia alibainisha katika Jimbo la Karatu kumekuwa na changamoto ya barabara kwa kipindi cha muda mrefu na kuwaahidi kuwa iwapo watampa nafasi ya kuwawakilisha bungeni atahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami.
"Najua hapa Mang'ola wananchi wengi wanategemea kilimo cha umwagiliaji na tatizo lao kubwa ni uhaba wa visima pamoja na miundombinu ya umwagiliaji,nadhani mnanijua mimi mwenyewe ni mkulima mkininipa kura matatizo yote haya nawahidi nitayamaliza,"amesema.
Wakati wa kumnadi mgombea ubunge huyo pamoja na kumuombea Rais kura Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Zelothe Steven Zelothe amesema kuwa, wamchague Rais Magufuli kwa kuwa ni muadilifu,mtetezi wa wanyonge,mchapakazi,mwanamapinduzi wa kweli.

Pia amesema Magufuli ni kiongozi mpenda haki,anachukia rushwa na ni mtetezi wa yale anayoyaamini hivyo wasiache kumchagua na katika kipindi chake cha miaka mitano ametekeleza ahadi zake zote kwa vitendo.
Kwa upande wake mgombea udiwani wa Kata ya Qurus, Danstan Panga amewataka wananchi wa Karatu kumchagua mbunge huyo kwa kuwa kwanza ni mkazi wa jimbo lao pia ni mtoto wa mkulima hivyo ataweza kupeleka matatizo yao bungeni ili yaweze kutatuliwa.Zinazouwiana soma hapa.
"Ndugu Wanakaratu tumeongozwa na upinzami miaka 25 hapa, lakini hakuna maendeleo yoyote tulioletewa barabara ni mbovu,huduma za afya hatupati vyema ,shule za bweni kwa watoto wetu wa kike niseme tu 25 imetosha tunahitaji mabadiliko ninaomba tusifanye makosa ya nyuma,"amesema Panga.
Kwa upande wake Balozi Batilda Burian amewataka wananchi kuwapa kura za kishindo wagombea urais,ubunge na udiwani CCM ili wakaweze kuwaletea maendeleo.

Tags
Siasa