Mkoa
wa Geita kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Geita umeanzisha
Kijiji Maalum kwa ajili ya Maonyesho chenye ukubwa wa ekari 100 katika Mtaa na Kata ya Bombambili mjini Geita, anaripoti Robert Kalokola (Diramakini) Geita.
Moja ya jengo la utawala la Kituo cha Ukanda wa Mamlaka ya Uwekezaji Kiuchumi (EPZA) ambalo liko ndani ya Kijiji cha Maonyesho chenye ukubwa wa ekari 100.(Picha na Robert Kalokola/Diramakini). |
Kijiji
hicho kimetengwa kwa ajili ya maonyesho ya bidhaa za aina mbalimbali,
teknolojia pamoja na huduma kwa sekta mbalimbali ikiwemo kilimo,madini
na ujasiriamali.
Moja ya jengo la utawala la kituo cha Ukanda wa mamlaka ya Uwekezaji Kiuchumi (EPZA) ambalo liko ndani ya Kijiji cha Maonyesho chenye ukubwa wa ekari 100(Picha na Robert Kalokola/ Diramakini). |
Akizungumza
katika kikao cha wakuu wa wilaya kutoka Chato,Mbogwe na Geita
waliotembelea kijiji hicho,Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert
Gabriel amesema, kijiji hicho kitakuwa na maeneo yenye huduma kama benki,wanyamapori,burudani,kumbi za mikutano pamoja eneo la maonyesho.
Ameongeza
kuwa, kijiji hicho kimeanza kutumika rasmi mwezi huu kwa ajili ya
Maonyesho ya Teknolojia ya Madini ambayo yameanza Septemba 17, mwaka huu
na yanatarajiwa kuhitimishwa Septemba 27, mwaka huu.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel amesema kuwa, eneo hilo
litakuwa na majengo mbalimbali na maeneo ya vivutio vingine.
Amesema
kuwa,kwa kuanzia,mwaka huu kwenye hayo maonyesho ya teknolojia ya
madini wanyama kama simba na chui ili watu waweze kushuhudia wanyama
hao.
Wakuu wa wilaya
kutoka Wilaya ya Chato ni Mhandisi Charles Kabeho,Wilaya ya Mbogwe Matha
Mkupasi na Fadhili Juma Mkuu wa Wilaya ya Geita ambao wamefika kwa
ajili ya kushuhudia maonyesho hayo.
Mkuu
wa Wilaya ya Geita, Fadhili Juma amewaomba wajasiriamali wanaopata
semina katika kijiji hicho kutoka NBC kutumia mafunzo hayo kwa vitendo
baada ya mafunzo ili yawasaidie kukuza vipato vyao.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel
akifafanua jambo katika mafunzo kwa wachimbaji na wajasiriamali wa Mkoa
wa Geita. (Picha na Robert Kalokola/Diramakini). |
Jengo
la EPZA la utawala katika kijiji hicho linajengwa chini ya ufadhili wa
fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) kutoka Mgodi wa kuchimba Dhahabu wa
Geita (GGML) kwa usimamizi wa Halmashauri ya Mji wa Geita.
Maonyesho
ya teknolojia ya madini na uwekezaji katika Mkoa wa Geita yalikuwa yanafanyika katika kiwanja cha CCM Kalangalala kwa awamu mbili.
Hii
ni awamu ya tatu ya maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya
kwanza katika Kijiji cha Maonyesho kilichopo chini ya Halmashauri ya mji
wa Geita ikiwa ni mojawapo ya miradi yake maalum ya uwekezaji kwa ajili
ya kukuza mapato ya halmashauri hiyo.