Grace Kiwelu:Wanavunjo msifanye makosa,Mimi,madiwani CHADEMA, Mgombea Urais Tundu Lissu tunatosha,tunajua tabu mnazopitia

GRACE Sindato Kiwelu ambaye ni mgombea Ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo la Vunjo ameangua kilio jukwaani akielezea tukio la kupigwa risasi na watu wasiojulikana kwa aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki na ambaye kwa sasa ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tundu Lissu.

"Ndugu zangu wananchi wa jimbo la Vunjo kata ya Mwika Kusini, napatwa na uchungu nikikumbuka jinsi kiongozi wetu alivyotaka kupoteza maisha huku akipigania maisha yenu ninyi...tumpe ridhaa awe rais nishirikiane naye kuboresha maisha yenu,"amesema.
Akinadi sera katika Kata ya Mwika Kusini, Kiwelu amesema iwapo atapata ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha wananchi wote wanapata bima ya afya bila malipo.

Mgombea huyo amesema kupitia, serikali mpya itakayoundwa na mgombea Urais wa Chadema, Tundu Lissu, imekusudia kutumia vyanzo mbalimbali vya mapato kuhakikisha watanzania wananufaika na bima hiyo ili kuwaondolea adha wanayopata sasa.

Amesema asilimia kubwa ya wananchi wanashindwa kumudu gharama za matibabu huku baadhi yao wakipoteza maisha.

Kuhusu suala la elimu bila malipo, Mgombea huyo amesema serikali itakayoundwa na Chadema ambapo yeye atakuwa miongoni mwao watahakikisha inatolewa kwa ubora ili wahitimu wawe ni watu wenye kujitegemea baada ya kumaliza na si kusubiri ajira serikalini.

Amesema, mpango ni kuhakikisha wazazi hawachangishwi fedha kwa ajili ya kulipia walimu kwa yale maeneo ambayo hayana walimu kama inavyofanyika kwa baadhi ya maeneo.

Kiwelu amesema atahakikisha makundi ya vijana, wanawake na wenye ulamavu wananufaika na asilimia 10 ya mikopo inayotolewa na halmashauri za wilaya nchini ili waweze kuanzisha miradi ya kiuchumi kuliko hali ilivyo sasa.

Naye mgombea udiwani wa kata hiyo ambaye anatetea tena nafasi yake, Charles Kawiche amesema kwa kipindi chake alifanikisha kupatikana kwa zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya shughuli za maenedeleo.

Mgombea huyo ameomba wananchi kumpa ridhaa tena ya kuwa diwani wao ili aweze kufanikisha baadhi ya miradi ambayo tayari ipo katika michakato mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news