Hawa ndiyo wagombea Urais, Ubunge na Udiwani waliopo 'matatani'

Photo credit:(Ujasusi.com)
Moja ya sifa kuu ya mgombea ambaye Watanzania wanamuhitaji kwa sasa ni yeyote ambaye atajikita katika kunadi sera za chama, kugusia yanayowakabili, kujenga hoja ambazo hazina viashiria vya chuki, ubaguzi au viashiria vya uvunjifu wa amani badala yake kutumia muda mwingi kueleza namna ambavyo atatekeleza aliyoyaainisha na kutoa nafasi ya kila mmoja kuuliza panapostahili ili kupata ufafanuzi wa kina kutoka kwa mgombea.Tume ya Uchaguzi wanasemaje kuhusu sifa za mgombea? Tizama video hii hapa chini.
Mgombea wa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani ambaye anaendelea na hekaheka za kampeni kwa sasa inamaanisha alikidhi vigezo vyote vya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kulingana na maelezo ya mtaalam hapo juu, hivyo sasa ni wakati wa kunadi sera ili wananchi wakikuelewa na kukubali uweze kuwa miongoni mwa wawakilishi wao baada ya Oktoba 28, mwaka huu ambayo ndiyo siku rasmi ya Uchaguzi.Je? Kejeli, maneno ya chuki, ubaguzi, kashfa au uchochezi wenye viashiria vya uvunjifu wa amani vitaweza kukuvusha Oktoba? Rejea video ya Kwanza, jibu ni hapana, Diramakini Business Limited (www.diramakini.co.tz) inakushauri ndugu mgombea usiwe chanzo cha kujikosesha kura au ushindi kwa kutumia hoja dhaifu, jikite katika hoja zinazogusa maisha ya Watanzania, achana na maisha ya watu binafsi, hoja za chuki na uchochezi ambazo ni hatarishi kwa unaotaka kuja kuwaongoza na usalama wa Taifa, rejea video zote, tafakari ujumbe, omba Mungu msamaha ulipoteleza, jisahihishe, anza safari upya, Mungu atakushindia. Ujumbe huu umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri Mtendaji wa Diramakini Business Limited,
(diramakini@gmail.com). Tunawatakia wagombea wote kila la heri, tuzingatie utu,umoja, amani na mshikamano wetu kama Taifa, baada ya Uchaguzi Mkuu tutaendelea na maisha yetu kama kawaida, ikiwa ni jadi yetu ya enzi na enzi ya kupendana.

 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news