Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) kwa mwaka 2019 imetangaza majina ya wateule 54 wanaowania tuzo hizo katika makundi 21.
Kati ya wateuliwa hao 25 ni kutoka magazeti, tisa kutoka redio , wanne kutoka runinga, Kati ya wateule hao, 24 ni wanawake - saba wakiwa wanatoka kutoka kwenye magazeti, mmoja kwenye vyombo vya habari vya mitandaoni na 16 kutoka vyombo vya kieletroniki wakati wateule wanaume ni 30 ambapo 17 kati yao ni wa magazeti na wanane ni wa vyombo vya eletroniki na wanne wa vyombo vya habari vya mitandaoni.
Jopo la Majaji liliongozwa na Pudenciana Temba. Majaji wengine ni Mohammed Kissengo, Imane Duwe, Khalfan Said, Mkumbwa Ally na Pili Mtambalike ambaye alikuwa katibu wa jopo hilo.
Washindi wa tuzo hizo watajulikana rasmi katika kilele cha Tuzo za EJAT kitakachokuwa Septemba 28,2020 katika hoteli ya Tanga Beach Resort, mjini Tanga ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Martin Shigela.
Jumla ya kazi 450 ziliwasilishwa kwa EJAT 2019. Kati ya hizo 192 ni kutoka magazeti wakati wanahabari wa redio na ruinnga waliwasilishwa kazi 250 na vyombo vya habari vya mitandaoni kazi nane.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Maandalizi ya EJAT, Kajubi Mukajanga imeeleza kuwa kwa waandaji wa EJAT – Baraza la Habari Tanzania na washirika , mwelekeo huu ni mzuri licha ya matatizo yaliyokuwepo kwa kuwa wanahabari wengi zaidi wanaenzi na kuthamani EJAT, ambayo safari hii ni ya mwaka wa 11, kama kipimo muhimu kwa umahiri wa uandishi wa habari.
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT ni Baraza la Habari Tanzania ambalo ni Mwenyekiti, Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Taasisi yaHhabari ya Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-Tan), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), HakiElimu, ANSAF, Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na SIKIKA.
Ifuatayo ni orodha ya wateule kutoka vyombombali vya habari,
WATEULE WA EJAT 2019
1 Neema Goyayi AFM Radio Dodoma
2 Fatma Abdallah Chikawe AZAM TV Dar es Salaam
3 Amina Semagogwa Radio Kwizera Kagera
4 Sauli Gilliard Daily News Dar es Salaam
5 Editha Karlo Mtanzania Kigoma
6. Zuhura Juma Said Zanzibar Leo Zanzibar
7 Idi Juma Afya Radio Mwanza
8 Yohani Gwangway Radio SAUT Mwanza
9 Dominic Mrimi Radio SAUT Mwanza
10. Gwamaka Alipipi Nipashe Dar es Salaam
11 Halili Letea The Citizen Dar es Salaam
12. Alfred Lastek Mushi Habari Leo Dar es Salaam
13. Sanula Athanas Sanula Nipashe Dar es Salaam
14 Baraka Jailosi Messa Habari Leo Songwe
15. Asha Ahmed Omar Chuchu FM Zanzibar
16 Hilda Phoya Mlimani TV Dar es Salaam
17 Agnes J. Almasy ITV Dar es Salaam
18 Deogratias Damian Macha Fountain Radio Kilimanjaro
19 Kelvin Matandiko Mwananchi Dar es Salaam
20. Kareny Masasy Habari Leo Shinyanga
21 Evanc Ng’ingo Habari Leo Dar es Salaam
22 Anord Jovine Kailembo Radio Kwizera Kagera
23 Agnes Mbapu TBC1 Dar es Salaam
24 Adella Herry Tillya EFM Radio Dar es Salaam
25 Betty Tesha TBC Taifa Dar es Salaam
26 Khamis Suleiman Said Channel 10 Dar es Salaam
27 Jamaly Hashim Said Azam TV Dar es Salaam
28 Essau Kalukubila Radio Jamii Micheweni Pemba
29 Joseline Joseph Kitakwa TBC FM Dar es Salaam
30 Isidory Peter Mtunda Pambazuko FM Ifakara, Morogoro
31 Ashton Balaigwa Nipashe Morogoro
32 Faraja Sendegeya Azam TV Dar es Salaam
33 Adam G. Hhando CG FM Tabora
34 Kija Yunus Mohamed Clouds TV Dar es Salaam
35 Regina Kulindwa Radio Sauti Mwanza
36 Agnes Anderson AFM Radio Dodoma
37 Rehema Mwaikema Azam TV Mwanza
38 Husna Mohammed Khamis Zanzibar Leo Zanzibar
39 Rehema Goodluck Mwananchi Dar es Salaam
40 Lucas Raphael Habari Leo Tabora
41 Marco Maduhu Nipashe Shinyanga
42 Sifa Lubasi Habari Leo Dodoma
43 Harriet Makweta Mwananchi Dar es Salaam
44 Godfrey Kahango Mwananchi Dar es Salaam
45 Rahma S. Ali Zanzibar Leo Zanzibar
46 James Kandoya The Guardian Dar es Salaam
47 James Kamala Daily News Dar es Salaam
48 Crispin Samson The Guardian Dar es Salaam
49 Hadija Omar Nassor Voice of Tabora Tabora
50 Aurelia Palali Kwizera radio Kagera
51 Abdul Kingo Nipashe Dar es Salaam
52 Muhidin Msamba The Guardian Dar es Salaam
53 Bakar Masoud Bakar Chuchu FM Zanzibar
54 Rajab Mustapha Mrope Pangani FM Pangani, Tanga
Makundi yaliyoshindaniwa ni :
1. Tuzo ya Kuripoti Biashara Uchumi na Fedha
2. Tuzo ya kuripoti Utamaduni na Michezo
3. Tuzo ya Kuripoti Kilimo na Biashara ya Kilimo
4. Tuzo ya Kuripoti Elimu
5. Tuzo ya Kuripoti Utalii na Uhifadhi
6. Tuzo ya Kuripoti Habari za Uchunguzi
7. Tuzo ya Uandishi Habari wa Data
8. Tuzo ya Kuripoti Haki za Bianadamu na Utawala Bora
9. Tuzo ya Mpiga Picha Bora
10. Tuzo ya Mpiga Picha Bora wa Runinga
11. Tuzo ya Mchora Vibonzo Bora
12. Tuzo ya Kuripoti Jinsia
13. Tuzo ya Kuripoti Wazee
14. Tuzo ya Kuripoti Watoto
15. Tuzo ya Kuripoti Usimamizi wa Mafuta, Gesi na Uchimbaji Madini
16. Tuzo ya Kuripoti Afya ya Uzazi
17. Tuzo ya Kuripoti Ubunifu wa Maendeleo ya Binadamu
18. Tuzo ya Kuripoti Athari za Kemikali kwa Afya na Mazingira
19. Tuzo ya Kuripoti Usalama Barabarani
20. Tuzo ya Kuripoti Hedhi Salama
21. Tuzo ya Wazi