Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt.John Magufuli wakati akihutubia maelfu ya wananchi (hawapo pichani mkoani Singida leo. |
SERIKALI ya Awamu ya Tano imetekeleza na inatarajia kutekeleza baada ya Oktoba 28, mwaka huu, hayo yamethibitika leo kutokana na hotuba za mgombea urais Dkt.John Magufuli.Baadhi ya mambo muhimu yaliyosemwa katika mkutano wa mgombea uyrais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania, Dkt. Magufuli leo Septemba 1, 2020 ni pamoja na;
1:Shilingi bilioni 470.4 zimetumika kutekeleza miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Singida.
Wananchi wakimfuatilia mgombea Urais,Dkt.Magufuli mjini Singida. 2:Serikali yake imejenga vituo vya afya vilivyowezesha akinama 730 kufanyiwa upasuaji hivyo kuokoa maisha yao na watoto wao.
3:Hospitali tatu za wilaya zimejengwa katika Wilaya za Mkalama, Ikungi na Singida.
4:Katika kipindi cha miaka mitano viwanda zaidi ya 8,500 vimejengwa.
5:Ajira milioni sita zimezalishwa katika kipindi cha miaka mitano na katika kipindi cha miaka mitano ijayo watazalisha ajira milioni nane.
6:Shilingi bilioni 52.6 zimetumika kujenga miundombinu ya shule yakiwemo madarasa, maabara na miundombinu mingine.7:Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida iko hatua za mwisho kukamilika ikiwa ni hatua mojawapo ya kuboresha sekta ya afya.
Wananchi wakimfuatilia mgombea Urais,Dkt.Magufuli mjini Singida. 8:Kulikuwa na vijiji 2018 tu vilivyokuwa vimefikishiwa umeme mwaka 2015, lakini katika miaka mitano vijiji 9570 vimefikiwa kati ya vijiji 12280 nchi nzima.
9:Shilingi bilioni 310 zimetumika kujenga miundombinu wezeshi.
10: Shilingi bilioni 27.2 zimetumika kutekeleza miradi ya maji ipatayo 66.
11:Uandikishaji wanafunzi umeongezeka kutoka milioni 1 hadi milioni 1.6 baada ya kuanza kwa mpango wa elimu bure.
12:Shilingi bilioni 17 zimetumika kujenga barabara za Singida mjini na kuziwekea taa.
13:Ujenzi wa barabara ya Chaya Singida hadi Tabora imebaki kilomita 20 kukamilika.
14:Vituo vya afya 487 vimejengwa Tanzania nzima.
Wananchi wakimfuatilia mgombea Urais,Dkt.Magufuli mjini Singida. 15:Serikali inajenga bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere litakalozalisha megawati 2,115.
16:Vijiji 9,570 vimefikiwa na nishati ya umeme ikilinganishwa na vijiji 2,018 vilivyokuwa na umeme mwaka 2015.
17:Bajeti ya Wizara ya Afya imeongezwa kutoka shilingi bilioni 30 hadi shilingi bilioni 270.
18:Rais Magufuli amewaambia wananchi yupo mbele zao kwa unyenyekevu mkubwa kuomba kura za vyama vyote kwa sababu maendeleo hayana chama.
19:Visima vinne virefu vimechimbwa kuongeza upatikanaji wa maji.
20:Shilingi bilioni 66 zimetumika kutekeleza miradi ya maji na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kutoka asilimia 41 hadi 54.21:Shule kongwe ikiwemo Mwenge Sekondari zimekarabatiwa ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha sekta ya elimu nchini.
22:Ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 850 hadi zaidi ya shilingi Trilioni 1.5.
23:Tozo 114 zimefutwa katika sekta ya kilimo na wafanyabiashara ndogondogo wamefutiwa kodi 54.
24: Kwa mujibu wa ripoti ya "Global Peace Index" Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki, ya 6 Afrika na 52 duniani kwa amani.
25:Mitandao ya simu imeimarika nchi nzima.
26:Serikali imejenga ukuta wa kilomita 25 eneo la Mererani ambao umesaidia kudhibiti wizi wa madini ya Tanzanite na upotevu wa mapato ya nchi.
"Tunamshukuru Mungu kwa kutuepusha na janga la Corona kutokana na maombi tuliyofanya kama taifa. Hii imetoa somo kubwa kwa mataifa mengi duniani kuwa Mungu anaweza,"ameyabainisha Rais Magufuli na mgombea kupitia CCM leo mjini Singida.