HAYA NI MAJINA YA WANAFUNZI WOTE WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO AWAMU YA PILI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amesema kuwa wanafunzi 7,586 kati ya 8,603 waliokosa nafasi awamu ya kwanza wamechaguliwa kijiunga na kidato cha tano katika awamu ya pili,anaripoti ANGELA MSIMBIRA OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akitoa taarifa juu ya uchaguzi huo leo.PICHA NA OR-TAMISEMI.

Akitoa taarifa kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha tano awamu ya pili leo, Waziri Jafo amesema kati ya wanafunzi waliochanguliwa ambao ni asilimia 88.18 ya waliokosa nafasi awamu ya kwanza walikuwa wasichana 1,109 na wavulana ni 6,477.

 
Amefafanua kuwa, baada ya kukamilika kuchagua wanafuzi wa kujiunga kidato cha tano awamu ya kwaza, wanafunzi 8,603 wakiwemo wasichana 1,281 na wavulana 7,322 hawakupangiwa shule.
 
Waziri Jafo amesema, wanafunzi 355 ikiwa ni wavulana 254 na wasichana 101 wamebadilishiwa kutoka vyuo mbalimbali na kujiunga na masomo ya kidato cha tano.Bonyeza hapa majina yote yapo kidao cha tano, vyuo vya ufundi na vyakati.
 
Amesema, kati ya wanafunzi waliochaguliwa, wanafunzi 615 wamepangiwa tahasusi za sayansi na hisabati na wanafunzi 6,971 wamepangiwa tahasusi za masomo ya sanaa na biashara.
 
Aidha, Waziri Jafo amesema jumla ya wanafunzi 1,017 wakiwemo wasichana 172 na wavulana 845 sawa na asilimia 11.82 wamekosa tahasusi zinazokidhi vigezo, hivyo kushindwa kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika awamu ya pili.
 
“Wanafunzi waliokosa nafasi za kujiunga na masomo ya kidato cha tano kwa kukosa tahasusi zinazokidhi vigezo wanashauriwa kuomba nafasi za masomo katika vyuo vinavyosimamiwa na NACTE,”amesisitiza Waziri Jafo.
 
Aidha Waziri Jafo amewataka wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano awamu ya pili kuhakikisha wanafika shuleni kuanzia Septemba 6 hadi 20, mwaka huu ambapo mwanafunzi atakeyeshindwa atakuwa amepoteza nafasi yake.Bonyeza hapa kupata orodha ya waliochaguliwa awali 
 
Hata hivyo kwa orodha ya majina yote ya chaguo la pili, Bonyeza hapa

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news