KATI ya tarehe 10.08.2020 hadi tarehe 01.09.2020 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako dhidi ya watuhumiwa wa makosa mbalimbali katika maeneo ya Ilemi, Ilomba, Iyunga, Iwambi, Forest, Iyela, Maanga, Mwanjelwa pamoja na Mabatini. Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,SACP Ulrich O.Matei.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA MATUKIO YA UPORAJI.
Jumla ya watuhumiwa saba walikamatwa maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambao ni-
⦁ KELVIN MAJEMBE GAWANGA [26] Mkazi wa Ilemi.
⦁ YOHANA MEDI DUZU [23] Mkazi wa Ilemi Masewe.
⦁ SEIF SAMSON SESO [32] Mkazi wa Ilemi Juhudi.
⦁ BEN JOSEPH JAMES @ MWAKALOBO [27] Mkazi wa Ilemi Kanisani.
⦁ RIZIKI MWAKAJINGA NJAGAJA [24] Mkazi wa Ilemi Masewe.
⦁ HAMIS MEJA [19] Mkazi wa Airport ya zamani.
⦁ KELVIN PASCHAL [28] Mkazi wa Makunguru.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA WIZI KWA NJIA YA MTANDAO.
Jumla ya watuhumiwa 11 kati yao mwanamke mmoja walikamatwa kwa makossa ya kujihusisha na wizi kwa njia ya mtandao kwa kulaghai watu na kujipatia pesa. Watuhumiwa hao ni:-
⦁ PAUL MASHAKA MZOPOLA @ BARIKI [22] Mkazi wa Mwakibete.
⦁ LACKSON KANYIKA MITSON [30] Mkazi wa Magege Ilemi
⦁ BOAZ GIDION KAPONDA [27] Mkazi wa Ituha
⦁ WILLE JACKSON KABOJELE [30] Mkazi wa Hasanga Uyole
⦁ STEPHEN ELSON MWAMPAMBA [23] Mkazi wa Mwakibete
⦁ ZAWADI JAKOBO MWASUMBI [32] Mkazi wa Gombe Uyole
⦁ FESTO GEORGE NDONDO [32] Mkazi wa Itezi Uyole
⦁ NOAH ALBANUS MKINDA [30] Mkazi wa Mwambene
⦁ PRISCA YOHANA JACKSON [20] Mkazi wa Gombe Uyole
⦁ SHUKURU GAWELO MSONGOLE [36] Mkazi wa Ituha.
⦁ LEMON JULIUS MKONDYA [36] Mkazi wa Ilemi Mapelele
Aidha watuhumiwa hao walikutwa na simu 19 za aina mbalimbali pamoja na laini zake ambazo zimesajiliwa kwa majina ya watu wengine.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA MATUKIO YA UVUNJAJI NA WIZI KWENYE MAHOTELI.
Jumla ya watuhumiwa 05 walikamatwa maeneo mbalimbali kwa tuhuma ya makosa ya uvunjaji na wizi katika Mahoteli Jijini Mbeya. Watuhumiwa hao ni:-
⦁ OSCAR AFWILILE MBEMBELA [20] Mkazi wa Magege Ilemi
⦁ ELSHA LUFINGO [23] Mkazi wa Ilemi Magege.
⦁ JOFREY BONIPAHCE MWAKAKIMA [23] Mkazi wa Magege Ilemi
⦁ AUGUSTINO GODFREY MASUBA [22] Mkazi wa Magege Ilemi
⦁ EMA KENEDY FRANCIS [20] Mkazi wa Makungulu.
Aidha walikamatwa watuhumiwa 04 wanunuzi na wapokeaji wa vitu / mali za wizi ambao ni:-
⦁ EMANUEL NJALI SOLO [54] Mkazi wa Ilolo Ruanda.
⦁ YUSUPH SICHEMA [28] Mkazi wa Tunduma.
⦁ YOHANA KASANGA [24] Mkazi wa Tunduma.
⦁ PAULO MBOLIGO [26] Mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya.
Watuhumiwa hao walikutwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni:-
⦁ TV Flat Screen aina ya Kodtec inchi 42
⦁ TV Flat Screen mbili aina ya Singsung inchi 32 na 28
⦁ TV Flat Screen aina ya TCL inchi 32
⦁ TV Flat Screen mbili aina ya Samsung inchi 50 na 19
⦁ TV Flat Screen aina ya Sundar inchi 19
⦁ TV Flat Screen mbili aina ya Sony inchi 32 na 28
⦁ Remote Control moja
⦁ Generator moja aina ya Boss
⦁ Spika kubwa mbili
⦁ Magodoro 02
⦁ Shuka 13
⦁ Mito ya kulalia 10
⦁ Redio 02 aina ya Aborder na Spika 05
⦁ Stendi za TV za kuchonga 06
⦁ Vipande 04 vya Kapeti
⦁ Mapazia 08
⦁ Simu 02
⦁ Jiko la Gesi 01 aina ya Taifa Gesi
Aidha watuhumiwa hao walikutwa na vifaa vya kuvunjia ambavyo ni:-
⦁ Mkasi Mkubwa 01
⦁ Plaizi 02
⦁ Bisibisi 01
⦁ Mikuki 02
⦁ Kipande cha Nondo 01
⦁ Glove ngumu jozi 01.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA MATUKIO YA UVUNJAJI NA WIZI KWENYE VYUO VIKUU.
Jumla ya watuhumiwa 04 wanaojihusisha na matukio ya uvunjaji na wizi katika vyuo vya elimu ya juu Jijini Mbeya walikamatwa. Vyuo hivyo ni SAUT, T.I.A na MZUMBE. Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
⦁ YUSUPH LAITON [22] Mkazi wa Ilemi
⦁ ONESMO NGEMELA [22] Mkazi wa Mabatini
⦁ VICTOR ANTHONY [23] Mkazi wa Forest ya Zamani
⦁ VICTOR DAVID [23] Mkazi wa Maanga
Aidha katika msako huu, watuhumiwa walikutwa na vitu/mali mbalimbali za wizi kama ifuatavyo:-
⦁ TV moja aina ya LG inchi 49
⦁ TV moja aina ya Star Times inchi 32
⦁ Laptop tatu aina ya DELL, HP na Accer
⦁ Meza moja ya Cherehani.
KUPATIKANA NA BHANGI.
Katika misako hiyo iliyofanyika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya jumla ya watuhumiwa 05 walikamatwa wakiwa na Bhangi Kete 136 wakiwa katika chumba kimoja wakivuta.
Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
⦁ EZEKIA BROWN BAHATI [17] Mkazi wa Ikoloti Lyoto.
⦁ VENANCE YASSIN BULILI [18] Mkazi wa Ilemi Masewe.
⦁ KULWA SADIKI JOHN [18] Mkazi wa Ilemi Juhudi.
⦁ DOTTO SADIKI JOHN [18] Mkazi wa Ilemi Juhudi.
⦁ HASSAN IDDI SAMWEL [20] Mkazi wa TEKU.
KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA TUKIO LA MAUAJI.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linwashikilia watuhumiwa wanne 1. KOLOSANI SAMSON [25] Fundi Ujenzi na Mkazi wa Mbalizi 2. HUSSEIN DICKSON [25] 3. ISAYA MWALUSANYA [30] na 4. SAID HASSAN [34] wote wakazi wa Mbalizi kwa tuhuma ya kosa la mauaji ya ANNAH PETER @ JOKOBO [51], Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na Mkazi wa Manga VETA Jijini Mbeya.
Ni kwamba mnamo tarehe 25.08.2020 majira ya saa 16:30 jioni huko mtaa wa Manga – Veta, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, ANNAH PETER @ JAKOBO [51], Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya alikutwa akiwa ameuawa kwa kuchomwa kisu tumboni, kifuani, sikioni, pajani na kwenye kitovu akiwa nyumbani kwake anapoishi peke yake.
Marehemu alitoka kazini tarehe 24.08.2020 majira ya saa 06:30 asubuhi na alitakiwa kuingia tena kazini saa 18:30 jioni lakini hakuonekana kazini hadi 25.08.2020 majira ya saa 16:30 jioni alipokutwa ameuawa ndani ya nyumba yake huko Manga Veta.
Kufuatia tukio hilo, kikosi kazi cha kuzuia na kupambana na uhalifu Wilaya ya Mbeya Mjini kilianza msako mara moja wa kumtafuta mtuhumiwa na mnamo tarehe 30.08.2020 majira ya saa 22:00 usiku huko Kijiji na Kata ya Iyula, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe alikamatwa KOLOSANI SAMSON [25] na baadae walikamatwa wenzake watatu kuhusiana na tukio hilo.
Chanzo cha tukio hilo ni kwamba mtuhumiwa alikuwa anadai fedha shilingi 500,000/= baada ya kufanya kazi ya kuremba madirisha 12 kwa makubaliano ya shilingi 50,000/= kwa kila dirisha katika nyumba ya marehemu na awali alilipwa kiasi cha shilingi 100,000/=. Siku aliyofuatilia deni lake nyumbani kwa marehemu alimkuta akiwa anaosha vyombo na alipomueleza madai yake ulizuka mzozo kati yao ndipo mtuhumiwa alimuua kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za mwili.
Aidha watuhumiwa wengine watatu wamekutwa na simu moja Smartphone aina ya Samsung mali ya marehemu. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA TUKIO LA MAUAJI.
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia METHOD KINYAMAGOA [25] Mkazi wa Kangaga Wilaya ya Mbarali kwa tuhuma ya mauaji ya mke wake aitwaye NEEMA MAPUNDA [25] Mkazi wa Kangaga.
Ni kwamba mnamo tarehe 04.08.2020 majira ya saa 10:30 asubuhi huko Kangaga, Kata ya Mawindi, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya, METHOD KINYAMAGOA [25] alimuua mke wake aitwaye NEEMA MAPUNDA [25] na kisha kukimbilia kusikojulikana.
Kufuatia tukio hilo, kikosi kazi cha kuzuia na kupambana na uhalifu Wilaya ya Mbarali kilianza kufanya ufuatiliaji na mnamo tarehe 01.09.2020 majira ya saa 12:00 mchana huko Mtaa wa Mama John, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya kikosi kazi hicho kilifanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa. Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
WITO WA KAMANDA.
Ninatoa rai kwa vijana kuacha tamaa ya mali kwa njia zisizo halali na badala yake wafanye kazi halali kwa ajili ya kujipatia kipato halali.
Aidha natoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya watu, kikundi cha mtandao wa watu wanaojihusisha na matukio ya wizi kwa njia ya mtandao kwa kukataa kulaghaiwa au kutapeliwa na kujikuta wanapata hasara au kupoteza mali zao kutokana na tamaa.
Pia naendelea kutoa rai kwa wanasiasa kufanya kampeni kwa amani na utulivu bila kuathiri shughuli nyingine. Jeshi la Polisi lipo imara na makini katika kipindi chote ili kuhakikisha amani na utulivu na halitasita kumchukulia hatua za kisheria mtu / kikundi cha watu kitakachofanya vurugu au kuonyesha viashiria vya uvunjifu wa amani.
Tags
Mahakamani