Isihaka Mchinjita:ACT Wazalendo tunakwenda kufanya makubwa kuanzia elimu,uvuvi,kilimo na uchumi

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Lindi, Isihaka Mchinjita (ACT-Wazalendo), amewaambia wananchi kuwa iwapo watampa ridhaa Oktoba 28,mwaka huu ataanza kushughulikia sekta ya elimu, uvuvi na kilimo ili kuharakisha maendeleo.

Ametoa ahadi hiyo leo katika mtaa wa Mnazimoja Manispaa ya Lindi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ubunge jimbo la Lindi.
Mgombea huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu amesema anatambua kwamba jimbo hilo lina changamoto nyingi.

 Amesema akichaguliwa na kuwa mbunge ataanza kushughulikia changamoto zilizopo kwenye sekta za kilimo, uvuvi na elimu.

Pia amesema wananchi wengi wa jimbo hilo wanategemea kilimo na uvuvi ili kujipatia vipato hivyo uwezo wa kuzisimamia zilete matokeo bora anao.

Kwani kwa sasa sekta hizo haziwanufaishi kutokana na usimamizi usioridhisha ambao unasababisha wananchi wawe na vipato duni ambavyo havilingani na kazi kubwa wanazofanya.

Amesema, wakulima hawalipwi bei za kuridhisha wanapouza mazao yao, kwani wanadhulumiwa. Amesema hata sekta ya uvuvi imehujumiwa nakusababisha maisha ya wavuvi kuwa magumu ingawa wanafanyakazi ngumu.

Kuhusu sekta ya elimu, mgombea huyo amesema jimbo hilo lina uhaba wa shule za msingi na sekondari. Hali inayotokana na waliokuwa wabunge wa jimbo hilo kutotambua umuhimu wa elimu kwa maisha na maendeleo ya wananchi.

Amesema jimbo hilo lina mitaa mingi huku shule zikiwa hazitoshelezi, hivyo watoto kukumbana na adha ya kutembea umbali mrefu.

Amebainisha kwamba mji wa Lindi hauna harakati za kiuchumi zenye tija na umedorora. Kwani shughuli zimekuwa ngumu kutokana na kutokuwa na viwanda ambavyo wafanyakazi na vibarua wa viwanda wangeweza kununua bidhaa za madukani, vyakula kungekuwa na wageni wengi ambao wangelala kwenye nyumba za kulala wageni.  Hivyo ni mambo ambayo yatapatiwa ufumbuzi mapema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news