Jaffar Salum Kibaya 35' ndiye aliyesababisha kilio kwa Ihefu SC, Mtibwa SC yaonja matokeo ya kwanza

Jaffar Salum Kibaya 35' amewapa ushindi wa 1-0 Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Ihefu SC Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mtibwa Sugar huu ni ushindi wa kwanza dhidi ya kocha Zubery Katwila baada ya sare mbili mfulilizo katika mechi zake mbili za awali nyumba.

Katika hatua nyingine Polisi Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania Uwanja wa Ushirika, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Daruwesh Saliboko alianza kuifungia Polisi Tanzania 32', Kelvin Kongwe Sabato akaisawazishia JKT Tanzania 64' na sasa kila timu imeshinda mechi moja, imefungwa moja na sare moja katika michezo yake mitatu hadi sasa.

Leo hatua ya tatu ya Ligi Kuu itaendelea kwa mechi mbili, Kagera Sugar wakiwakaribisha Yanga SC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na Tanzania Prisons wakiwa wenyeji wa Namungo FC Uwanja wa Mandela, Sumbawanga.

Kesho mabingwa watetezi, Simba SC watamenyana na Biashara United ya Musoma mkoani Mara na Coastal Union wataikaribisha Dodoma Jiji Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wakati Mbeya City watamenyana na Azam.

Hata hivyo,raundi ya tatu itakamilishwa Jumatatu kwa michezo mingine miwili, Ruvu Shooting na Gwambina Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Mwadui FC watawakaribisha KMC Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga, hadi sasa mambo hayajawa mazuri kwa wakongwe wa soka Tanzania, pengine mambo yanaweza kubadilika,hatujui, tuziachie 90' uwanjani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news