Jakaya Kikwete awataka waache kupotosha kuhusu mikoa ya Kusini

KAMPENI za kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka huu katika ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeendelea kupamba moto kila kona, huku wagombea kwa nafasi ya udiwani, ubunge na urais wakiendelea kunadi sera zao kwa namna tofautitofauti.

Pia baadhi ya vyama vimeendelea kuzindua kampeni kwa nafasi hizo kuanzia ngazi ya kata, jimbo na mkoa ambapo leo Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete ameongoza zoezi hilo mkoani Lindi. Taarifa mpya bonyeza hapa.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Kikwete.
             Wakati wa uzinduzi amesema, wanasiasa na wagombea wanaosema mikoa ya Lindi na Mtwara imesahauliwa na imeachwa nyuma kimaendeleo hawaijui mikoa hiyo na ni waongo ambao wanapaswa kupuuzwa.

Kikwete ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika Mkoa wa Lindi kwa wagombea wanaopitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao ulifanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Ilulu ndani ya Manispaa ya Lindi.

Rais huyo mstaafu amesema hakuna Mkoa wowote ambao una vitu vyote, kwani mambo ambayo yamefanyika katika mikoa hiyo yanaweza yasiwepo mikoa mingine. Vivyo hivyo,yaliyopo katika mikoa mingine hayapo katika mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara. 

Amesema, si kweli kwamba mikoa hiyo imeachwa nyuma na imesahauliwa, hivyo kwa namna moja au nyingine wanaosema hivyo huenda hawanaufahamu wa mambo au wanakusudia kupotosha kwa makusudi.

Mbali na hayo ametaja mambo mengi yaliyofanyika katika mikoa hiyo ikiwemo miradi ya maendeleo. Amesema wakati akiwa Katibu wa CCM wa wialaya Nachingwea mwaka 1986 ilikuwa si jambo la ajabu kusikia watu wameliwa na simba au kutembea bila kukutanana nyoka. Lakini kwa sasa Nachingwea imebadilika na ina maendeleo makubwa.

Akizungumzia kuhusu miundombinu katika mikoa hiyo amesema hali ya barabara ilikuwa mbaya. Hasa kutoka katika mikoa hiyo kwenda Dar es Salaa, lakini kwa sasa hakuna tatizo kama hilo.

Dkt.Kikwete amesema, kazi ya kuleta maendeleo kwa wananchi ni endelevu, kwani hata sasa mambo mengi yamefanyika na yanaendelea kufanyika kila siku kwa manufaa ya wananchi.

"Hivyo kun akila sababu ya wananchi kuchagua CCM kiendelee kuwa chama tawala kutokana na kusimamia na kuendeleza amani, utulivu na mshikamano. Mambo ambayo yanasababishwa na sera unganishi na jumuishi. Bila sera jumuishi na unganishi kungekuwa na migogoro tena mikubwa sana,"amesema Dkt.Kikwete.

Naye Mjumbe Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Lindi, Abass Matulilo amesema ni jambo lisilokubalika ndani ya mkoa huo kuruhusu wananunuzi wanaonunua korosho nje ya mfumo rasmi(kangomba) kwani kuruhusu wanunuzi hao ni kuruhusu wakulima wadhulumiwe, hivyo wote wenye mawazo ya kurudisha hali hiyo wapuuzwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news