MGOMBEA Ubunge katika Jimbo la Musoma Mjini kupitia Chama cha NCCR Mageuzi, Joyce Sokombi amesema, endapo atachaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu atahakikisha anasaidia kwa urahisi upatikanaji wa Kituo cha Afya Kata ya Buhare pamoja na kutatua kero ya maji kwa wakazi wa kata hiyo hususani kinamama ambao mara nyingi hupata adha hiyo, anaripoti AMOS LUFUNGULO (Diramakini) MARA.
Mbali na hilo, amesema atahakikisha anapigia kelele upatikanaji wa mikopo kwa wepesi na kutengeneza mazingira mepesi ya kupata mikopo hiyo, ili kuwawezesha kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo itakayozalisha kipato na kuwakwamua kiuchumi katika maisha yao.
"Naombeni mnichague kusudi nikatimize azima ya kuleta mabadiliko thabiti katika Jimbo la Musoma Mjini, nitahakikisha vikundi vya kinamama, walemavu na vijana vinapata mikopo kwa wepesi tofauti na sasa, pia naahidi kujenga bweni katika Shule ya Sekondari Buhare ili mabinti waondokane na adha ya kupewa ujauzito na kukatiza masomo yao. Sitaenda bungeni kulala bali kuwawakilisha wana Musoma Mjini kwa uhakika kusudi kuwasemea matatizo yenu,"amesema Sikombi.
Aidha, amesema endapo atashinda atakapofika bungeni, atawasilisha maombi ya waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Musoma cha MUTEX ili Serikali iweze kushughulikia malipo yao tangu kiwanda hicho kilipowapa barua za likizo bila malipo na hawakurejea tena kazini.
Kwa upande wake Kamishina wa NCCR Mageuzi Mkoa wa Dodoma, Fataa Amiri amewaomba wananchi wa Kata ya Buhare na Jimbo la Musoma Mjini kumchagua Sokombi aweze kuwawakilisha wananchi kuwasemea bungeni ili kutatua kero zinazowasibu.
Naye Monica Julius Meneja Kampeni wa Mbunge huyo amesema kuwa, wananchi wa Musoma Mjini wamchague Sokombi aweze kushughulikia tatizo la viwanda ambavyo vimekufa vianze kufanya kazi pamoja na kuharakisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, hasa kwa maeneo ya kata ambazo ziko pembezoni mwa Manispaa ya Musoma zinazokabiliwa na tatizo la maji.
"Wafanyakazi wengi waliokuwa wakifanya kazi kwenye kiwanda cha samaki cha Bukanga na MUTEX kwa sasa hawana ajira, tunahitaji mabadiliko tumchague Sokombi aende kuvisemea viwanda hivi kusudi Serikali ikivifufua vianze kufanya kazi, vikianza kufanya kazi ajira zitapatikana kwa kinamama, vijana na watu wote, na uchumi wa Musoma Mjini utaimarika tofauti na sasa, ichagueni NCCR Mageuzi ikatekeleze azima ya maendeleo ya Musoma Mjini,"amesema.
Aidha, amesema ipo changamoto ya mazingira ya kusomea kwa wanafunzi hasa wa shule za Msingi ikiwemo upungufu wa madawati na upande wa huduma hafifu za upatikanaji wa matibabu kwa wazee, ambapo amesema chama hicho kikichaguliwa kitaenda kufanya mabadikiko ya uhakika kwa maslahi mapana ya Wananchi wa Musoma Mjini.
Mbali na hilo, amesema atahakikisha anapigia kelele upatikanaji wa mikopo kwa wepesi na kutengeneza mazingira mepesi ya kupata mikopo hiyo, ili kuwawezesha kufanya miradi mbalimbali ya maendeleo itakayozalisha kipato na kuwakwamua kiuchumi katika maisha yao.
Joyce Sikombi akiomba kura kwa wananchi wa Kata ya Buhare katika mwendelezo wa kampeni zake za kuwania Ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini.(DIRAMAKINI). |

Tags
Siasa