Joyce Sokombi:Ilani ya NCCR Mageuzi imesheheni, hapa kero zote zitapata majibu na utatuzi,Musoma Mjini nipeni kura zote

NA FRESHA KINASA

MGOMBEA Ubunge katika Jimbo la Musoma Mjini kupitia Chama cha NCCR Mageuzi, Joyce Sokombi ameendelea na kampeni za kuomba kura na kunadi sera za chama hicho kwa wananchi katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka huu katika Mtaa wa Zanzibar kata ya Makoko
 
Amesema endapo atachaguliwa atawezesha ujenzi wa Shule ya Msingi katika Mtaa huo pamoja na uboreshaji wa barabara za mitaa ambazo zimeharibika ndani ya miezi sita.
Mbali na hilo, Sokombi amesema  atawezeshau ujenzi wa soko ndani ya kipindi cha miezi mitatu baada ya kuchaguliwa, kwani kwa sasa wananchi hufuata mahitaji yao nje na eneo lao jambo ambalo amesema yeye atakuwa na uwezo wa kutekekeza ahadi yake, pamoja na kuimarisha hali ya upatikanaji wa mikopo kwa Vijana, Kinamama, na Walemavu.
"Mkinipa ridhaa ya kunichagua nitatumia juhudi na nguvu zote kuhakikisha upatikanaji wa mikopo unakuwa mwepesi, nitasimamia kwa karibu usajili wa vikundi, ili kutengeneza uchumi bora kwa makundi yote ili kuyawezesha kujikwamua kiuchumi tofauti na sasa,"amesema.

Pia ameongeza kuwa, ataimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Mtaa wa Zanzibar na Kata ya Makoko kiujumla, kutokana na uwepo wa Ziwa Victoria karibu na mtaa huo pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kushughulikia kero za wananchi ambazo bado zinawakabili.

Naye Kamishina wa Chama cha NCCR Mageuzi,Fataa Amiri, amesema wananchi wa Musoma Mjini wanapswa kumchagua Sokombi kusudi atimize dhamira yake thabiti ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Musoma Mjini na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wote.

Neema Julius na Zuena Marwa wakazi wa Mtaa wa Zanzibar Kata ya Makoko wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema iwapo Sokombi atashinda na kuwezesha ujenzi wa soko katika mtaa huo, wataondokana na kwenda kufuata mahitaji muhimu mbali na eneo lao jambo ambalo wamesema ni hitaji la Msingi kwao.

"Tukiwa na soko katika Mtaa wetu tutaweza kufanya biashara ikiwemo kuuza matunda, nyanya, dagaa na vitu vingine Kinamama tutapata fedha na kuwa na uchumi imara katika familia zetu."amesema Khadija Musa.

Neema Paschal na Blandina Pius, wamesema wamepokea kwa shukrani ahadi ya Sokombi aliyoitoa ya kujenga Shule katika Mtaa wa Zanzibar ambapo wamesema itainua ufauru wa Wanafunzi tofauti na see, ambapo hulazimika kwenda kusoma katika Shule ya Msingi Nyarigamba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news