KMC, Azam FC, JKT Tanzania zachekelea matokeo Ligi Kuu Bara

MICHUANO ya Ligi Kuu Bara imeendelea kushika kasi baada ya Timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) kuuanza vema msimu kwa kuichapa mabao 4-0 Mbeya City.

KMC wameupata ushindi huo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Septemba 7, 2020 ambapo mabao hayo yalifungwa na Israel Mwenda, Hassan Kabunda, Abdul Hillary na Paul Peter.

Wakati hayo yakijiri mapema, kwa upande wa Uwanja wa Azam Complex ambao upo Chamanzi wilayani Temeke, Dar es Salaam bao pekee la mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa limetosha kuipa Azam FC ushindi wa moja kwa buyu dhidi ya Polisi Tanzania .

Mshambuliaji Chirwa alifunga bao hilo dakika ya 45 kwa kichwa akimalizia 'cross' kali ya mshambuliaji raia wa Zimbabwe, Prince Dube kutoka upande wa kushoto wa uwanja huo.

Aidha,JKT Tanzania imepata ushindi wa ugenini wa moja kwa ubuyu dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera ambapo bao hilo la pekee la Adam Adam dakika ya 16 lilitosha kufunga hesabu.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news