KMC FC kuivaa Mwandui FC kesho

Kikosi cha Timu ya ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kimejiandaa vilivyo katika kukabiliana na mchezo wake wa kesho dhidi ya Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga mchezo utakaopigwa katika Dimba la Mwadui Complex Mkoani humo,anaripoti Christina Mwagala kutoka KMC FC.

Kikosi hicho ambacho kimeweka kambi Mkoani humo leo kimefanya mazoezi katika uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga ikiwa ni katika hatua za mwisho kabla ya kuelekea kwa mchezo huo ambao KMC FC itakuwa mgeni dhidi ya Mwadui FC.

Katika kikosi hicho hali ya wachezaji ni nzuri na kwamba hakuna majeruhi ambaye anaweza kukosa mchezo huo ambao KMC imejipanga kuhakikisha kwamba inapata ushindi wa alama tatu kwa lengo la kuendelea kuongoza ligi kuu inayoendelea hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news