KMC FC YAENDELEA KUJIFUA KUELEKEA LIGI KUU DHIDI YA MBEYA CITY










 

Timu ya mpira wa miguu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imeendelea leo kujifua katika mazoezi yake ikiwa ni katika hatua ya kujiandaa na ligi kuu Tanzania Bara itakayoanza Septemba 6, mwaka huu.
Christina Mwagala ambaye ni Afisa Habari wa KMC FC amesema,katika msimu huo wa ligi, timu ya KMC FC itaanza mchezo wake wa kwanza siku ya Jumatatu ya Septemba 7, mwaka huu katika Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo itakuwa wenyeji wa mchezo huo dhidi ya Mbeya City kutoka mkoani Mbeya.

Kocha wa timu hiyo, Habibu Kondo amesema kuwa, kikosi chake kipo vizuri na kwamba wapo tayari kwa mtanange huo katika kuhakikisha kuwa wanakuwa mabingwa kwenye msimu wa ligi 2020/2021 .

Ameongeza kuwa, katika maandalizi hayo wameweza kuboresha kikosi hicho ikiwa ni pamoja na kurekebisha changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita na kwamba katika msimu huu timu hiyo imekuwa na maboresho makubwa.

Amefafanua kuwa, katika maandalizi hayo timu ya KMC FC imecheza michezo ya kirafiki nane ambayo ni dhidi ya timu za DTB Bank, Kagera Sugar, Namungo, JKT Tanzania, Polisi, Azam pamoja na Simba ambapo kupitia mechi hizo zimeiwezesha timu kujiweka sawa kwa ajili ya kuanza ligi kuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news