KMC FC YAIFUATA KAGERA SUGAR MKOANI KAGERA

Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara , KMC FC leo imeondoka mkoani Shinyanga kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya kukabiliana na timu ya Kagera Suger mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Kaitaba Septemba 25 saa nane kamili mchana,anaripoti Christina Mwagala,KMC FC.Timu hiyo imeondoka kwa usafiri wa basi na  itaweka kambi mara itakapofika na kwamba wachezaji watapumzika kabla ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo ambapo Kagera Suger  ni wenyeji.

Katika kikosi hicho hakuna majeruhi na kwamba wote wanahali nzuri hivyo wako tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ambapo Timu ya KMC FC inahitaji ushindi huo kwa ajili ya kuendeleza hari ya  kupata matokeo mazuri na hivyo kusalia kwenye nafasi ya kwanza.

Jana KMC FC ilicheza mchezo wake wa tatu dhidi ya Mwadui ambapo ilipata matokeo mazuri kwa kuifunga mabao mawili kwa moja na hivyo kurudi kweye nafasi ya kwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news