Timu ya KMC FC leo imeibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja dhidi ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga mchezo uliopigwa katika uwanja wa Mwadui Complex mkoani humo,
anaripoti Christina Mwagala (KMC FC).
Magoli hayo yamefungwa na Lusajo Reliant mnamo dakika 75 na 84 katika kipindi cha pili cha mchezo huo na hivyo kuibua shangwe za mashabiki wa timu hiyo ambao wamesafiri kutoka Dar es Salam na kuungana na wa mkoani Shinyanga.
KMC ilikuwa imejiandaa kwa mchezo huo kwa ajili ya kupata matokeo mazuri ambayo yataiwezesha kuendelea kuongoza ligi kuu soka Tanzania bara na kuishusha Azam.
Kwa matokeo hayo, KMC imeendelea kujiweka katika nafasi nzuri baada ya kushinda michezo yote mitatu tangu kuanza kwa ligi kuu msimu huu wa 2020/2021 Septemba 17,mwaka huu.
Tags
Michezo