Kuanzia Oktoba Mosi, 2020 vitambulisho vya NIDA, udereva,hati ya kusafiria na namba za simu kusajili wageni huduma za malazi nchini

Wageni wa ndani na nje ya nchi watakaolala kwenye huduma za malazi zilizosajiliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mujibu wa sheria kuanzia Oktoba 1, 2020 watatakiwa kuanza kusajiliwa kwenye mfumo wa kielektoniki wa MNRT PORTAL.

Wageni hao watatakiwa kuwa na Vitambulisho vya Taifa (NIDA) au Hati za Kusafiria na wale ambao hawatakuwa na vitambulisho hivyo watasajiliwa kupitia namba za simu au vitambulisho vya udereva

Muonekano wa miongoni mwa maeneo yenye sehemu za malazi bora kwa wageni kutoka ndani na nje ndani ya Jiji la Dar es Salaam. (Diramakini).
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja ya usajili wageni wanaolala kwenye huduma za malazi kupitia mfumo wa kielektoniki wa MNRT PORTAL kwa wamiliki wa malazi wapatao 200 wa Kanda ya Pwani.

Amesema, lengo kuu la kusajili wageni hao katika huduma hizo ni kupata taarifa zitakazosaidia Serikali kupata takwimu sahihi kwa ajili ya kuboresha sekta ya utalii nchini.

Amesema, taarifa hizo zitatumika kama nyezo katika kuanda sera,mikakati na mbinu katika kuboresha sekta ya utalii hasa utalii wa ndani ambao mwamko wake umekuwa mdogo kwa Wananchi
Amesema mfumo huo wa kusajili wageni utatumika katika mahoteli, kambi pamoja lodge pekee zinazotambulika na wizara hiyo.

Amesema, utaratibu huo wa kusajili wageni ni takwa la kisheria, hivyo amewataka wamiliki wa malazi hao kuhakikisha kuanzia tarehe 1, Oktoba mwaka huu wanaanza kutekeleza agizo hilo kwa kusajili wageni wanaofika katika huduma za malazi kwa kutumia vitambulisho hivyo.

Katika hatua nyingine, Kaimu Mkurugenzi, Chitaunga amewatoa hofu wamiliki wa malazi kuwa taarifa hizo za wageni zitatumika kwa ni kwa ajili ya matumizi ya serikali pekee na zitatunzwa kwa usiri wa hali ya juu.

Kwa upande wake, Samson Nelsa ambaye ni mmiliki wa Huduma za Malazi katika mkoa wa Pwani, amesema, mfumo huo utasaidia serikali kuandaa takwimu za idadi ya watalii.

Amesema, mfumo huo mbali ya kuisaidia Serikali kupata takwimu za utalii wa ndani na wa nje pia utasaidia wamiliki wa hoteli kuwa na sehemu salama ya kuhifadhia taarifa zao.

Naye Mohamed Juma ambaye ni mmliki wa Hoteli ya Rainbow licha ya kuipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kutaka kujua takwimu halisi ya watalii kupitia mfumo huo utakaoanza kutumika mwezi ujao ameitaka wizara hiyo kuhakikisha hakuna taarifa za wateja wao zinatumika kwa ajili ya maslahi binafsi

Aidha,ameitahadharisha wizara kuwa makini katika kuulinda mfumo huo ili usiweze kushambuliwa na baadhi ya watu wenye maslahi yao binafsi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news